Ajali mbaya kabisa katika daraja la Kawe

Picture
Ajali mbaya na ya kutisha imetokea leo alfajiri katikati ya madaraja mawili ya chuma yaliyoko eneo la Kawe pembeni ya kambi ya JKT Mlalakuwa, Dar es Salaam.

Ajali hiyo imesababisha dereva kupoteza maisha na kuacha vipande vya ubongo vikining’inia katika moja ya madaraja hayo, baada ya gari hilo aina ya Toyota Celica GTR lenye namba za usajili T220ABL kugonga na kisha kuingia kwenye ukingo wa daraja na kisha kutumbukia kwenye mto.  Maiti iliondolewa asubuhi wakati ajali hiyo ilitokea kati ya saa 8 na saa 9 alfajiri.

Habari kwa mujibu wa Imma Matukio blog (bofya hapa kuona picha zaidi). Picture

Post a Comment

أحدث أقدم