Waziri wa Habari, Utamaduni, na Michezo Dk Fenella Mukangala
amesema serikali imewaka mikakati ya kudhibiti haki za kazi za wasanii
wa muziki na filamu.
Akijibu hoja ya kamati ya maendeleo ya jamii bungeni jana, Dk Fenella
alisema nyimbo nyingi za wasanii zinazotumiwa katika vifaa vya
mawasiliano vinaendelea kuwanyonya wasanii kutokana na mikataba
waliyoingia wasanii.
“Kuna haja ya kukaa na wadau kuona kuna nini cha kufanya,” alisema Dk
Fenella. “Hata hivyo serikali kupitia urasimishaji ambao tumekwisha
uzungumza, imeaanda mikataba bora ambayo inayoonyesha bayana namna kazi
za filamu ama muziki zitakavyotumiwa katika mifumo ya
mawasiliano,itakayoomwezesha mhusika kupata haki yake stahiki. Basi
tunaomba wale wanaohusika wahakikishe wanatumia hizi sheria na
kuwasiliana na bodi ya filamu ili kazi zao ziwe katika hali nzuri.”
Pia alisema serikali imeanzisha utaratibu wa kubandika stempu za kodi
katika bidhaa za filamu na kazi za muziki ili kubaini kazi halali na
fake.
“Stamp hizo zinafanyika nje ya nchi hivyo siri za utengenezaji wake
haziingii mikononi msimo salama. Nasema hivi kwasababu ilijitokeza
wakati wa kuchangia zipo kazi ambazo zinazunguka na stamp bandia.

إرسال تعليق