
MWIMBAJI anayesadikika kuwa na
sauti tamu zaidi kwa sasa, Christian Bella kutoka Malaika Music Band, amesema
atashiriki tamasha la Gurumo litakalofanyika Jumamosi hii kwenye viwanja wa TCC
Club Chang’ombe.
Mratibu wa tamasha hilo, Juma
Mbizo amesema Christian Bella, ameomba awekwe kwenye ratiba ya waburudishaji
ambapo atapanda kuimba japo wimbo mmoja kama ishara ya kuonyesha kuukubali
mchango wa gwiji Muhidin Maalim Gurumo.
Kama ilivyoelezwa hapo awali,
tamasha la Gurumo, limeandaliwa mahsusi kwaajili ya kumuaga kwenye muziki wa
jukwaani baada ya kutangaza rasmi kustaafu.
Mbizo ameongeza kuwa Christian Bella amesema miongoni mwa kazi anazozikubali sana hapa nyumbani, ni kazi za Msondo Ngoma chini ya Gurumo.
إرسال تعليق