Stori: Haruni Sanchawa na Imelda Mtema
KIFO cha ghafla cha mtoto Suleiman Rajabu (17) aliyekuwa na tatizo la mguu mmoja kuvimba tangu utoto kilichotokea Desemba 6, 2013 nyumbani kwao, Kitunda-Kivule ‘Bombambili’, Dar kimeibua mengi, lakini zito ni ushirikina kuhusishwa, Uwazi limeambiwa.
KIFO cha ghafla cha mtoto Suleiman Rajabu (17) aliyekuwa na tatizo la mguu mmoja kuvimba tangu utoto kilichotokea Desemba 6, 2013 nyumbani kwao, Kitunda-Kivule ‘Bombambili’, Dar kimeibua mengi, lakini zito ni ushirikina kuhusishwa, Uwazi limeambiwa.
Suleiman ilikuwa apelekwe India kwa matibabu, Desemba 8, 2013. Maandalizi yote ya safari yalishakamilika.
Baadhi ya ndugu waliozungumza na Uwazi msibani hapo, walitoa sauti
zao wakituhumu kuwa kuna mkono wa mtu katika kifo hicho kutokana na
mazingira yake.
Ndugu mmoja ndani ya wanafamilia ambaye hakutaka jina lake liandikwe
gazetini alisema kilichomsukuma kunena hayo kwa ujasiri ni kuona kwamba
mtoto huyo alizaliwa na tatizo hilo, sasa ana miaka 17 na katika muda
wote familia ilihangaika kutafuta tiba, “iweje leo, siku moja kabla ya
kusafirishwa kwenda India kwa matibabu ndiyo afariki dunia?
“Kufa kupo lakini kwa Suleiman aliyeishi kwa mateso kwa miaka kumi na
saba mpaka juzijuzi tu Kampuni ya Global Publishers ikaandika habari
zake na watu wakamsaidia mtoto, iweje afe siku moja tu kabla ya safari?”
alihoji ndugu huyo.
Waombolezaji wengi waliokutwa msibani hapo pia nao walizungumzia uwezekano wa ushirikina kuhusishwa.”
Habari za ugonjwa wa mtoto huyo zilikuwa zikiandikwa na Magazeti
Pendwa ya Global Publishers ambapo picha yake pia ilionesha jinsi mguu
mmoja ulivyovimba kimaajabu na kumfanya ashindwe kutembea maishani
mwake.
Familia yake iliomba msaada kwa wasamaria wema ili mtoto huyo
atibiwe. Awali baada ya kupata kiasi cha fedha, alipelekwa Hospitali ya
CCBRT ya jijini Dar ambako walishauri apelekwe India.
Mmoja wa watu walioguswa na kumlilia mtoto huyo kabla na baada ya
kifo ni mtangazaji wa televisheni wa kituo cha Channel Ten ambaye pia
ni Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu ambaye pamoja na masikitiko yake
alianzisha utaratibu wa kutafuta njia za kumsaidia mgonjwa huyo
kupitia kipindi chake cha Mimi na Tanzania kinachorushwa hewani na
Runinga hiyo na kutoa misaada mbalimbali ya hali na mali.
Kupitia kipindi hicho na magazeti ya Global, michango iliyokusanywa
ili kumsaidia ilifikia shilingi milioni 13 ambapo sehemu ya fedha hizo
zilishalipwa kwenye Hospitali ya Ganga, India ambako marehemu ilikuwa
apelekwe kwa matibabu Jumapili iliyopita.
Mratibu
wa safari iliyokufa ya Suleiman, Imelda Mtema ambaye ni mwandishi wa
habari wa Global Publishers alisema juzi kuwa, kwa vile fedha za
kumlipia marehemu zilishalipwa India na haziwezi kurudishwa, mtoto
Hamis Hashim ambaye naye ana tatizo kama la marehemu Suleiman atapelekwa
nchini humo kutibiwa.
Baba mzazi wa Suleiman, Rajabu Upinde aliwashukuru wote walioguswa
na mwanaye hasa walioendesha harakati za kufanikisha michango ya mtoto
huyo lakini akasema haikuwa riziki.
Mazishi ya Suleiman Rajabu yalifanyika Desemba 7, mwaka huu
Mwaneromango, wilayani Kisarawe mkoani Pwani. Mungu ailaze pema peponi
roho ya marehemu. Amina.
-GPL
إرسال تعليق