Dar es Salaam — Zikiwa
zimepita siku kadhaa baada ya kumalizika kwa mafanikio maonesho ya
mitindo ya Swahili Fashion week, mdhamini wa maonesho hayo kampuni ya
mawasiliano ya Vodacom Tanzania imeahidi kuendelea kuwaunga mkono
wanamitindo nchini na kuwasaidia kufikia malengo yao.
Akizungumzia mafanikio katika maonesho hayo, Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya Umma na Mawasiliano wa Vodacom

Tanzania, Joseline Kamuhanda amesema kampuni yake imekuwa mdau mkubwa katika kuwaunga mkono wanamitindo nchini.
“Ubunifu wa mitindo ya mavazi imekuwa ni ajira kwa mamia ya Watanzania ambayo inawalipa vizuri tu, inavutia kuona tasnia hiyo ikikua kwa kasi ya ajabu huku sisi tukiwa ni sehemu ya ukuaji huo. Siku zote tumekuwa tukiunga mkono shughuli hizi nchini na ninaahidi kuendelea kufanya hivyo kwani kwa pamoja tukishirikiana sisi na wabunifu wetu ndipo tunaweza kuitangaza nchi yetu katika ulimwengu wa wabunifu.” Alisema Kamuhanda.

Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya
Umma na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Joseline Kamuhanda (kushoto)
akikabidhi Tuzo ya Programu bora ya fasheni ya mwaka kwa waongoza
kipindi cha “NIVARNA” kinachorushwa na EASTV
Aliongezea
pia “kuna watu wengi wenye vipaji na wanahitaji udhamini wetu ili
kupata fursa ya kudhihirisha uwezo wao. Tumejidhatiti kufanya nao kazi
bega kwa bega kuhakikisha hilo linafanikiwa, tunawaomba na wao waongeze
bidii kuwa wabunifu zaidi kwa kubuni mavazi ambayo si yatawatagaza wao
bali na taifa kwa ujumla.” Alisema Kamuhanda na kumalizia kuwa
“Tunanataka ifikie hatua nchi yetu inakuwa ni sehemu ya wanamitindo
mbalimbali kujifunzia, vilevile nawaomba watanzania waunge mkono kazi za
nyumbani, tuachane na kuthamini vya watu tujaribu kuwa wazalendo
zaidi.”
Robert Harrison ambaye alikuwepo siku ya maonesho hayo alisifu jinsi tamasha hilo lilivyafanyika na kupongeza kwa kiasi kikubwa juhudi zilizofanywa na waandaaji kwa kushirikiana na wadhamini wao.
“Nimefurahi sana kuhudhuria tukio hili, nimevutiwa sana na uwezo wa wabunifu wetu wa nyumbani kwa kweli sasa tunaweza kushiriki kimataifa na kushinda. Kwa dunia ya sasa hivi muonekano na mpangilio wa kimavazi una nafasi yake katika maisha yetu. Ninapenda kuvaa na kuonekana nadhifu lakini siwezi kufanikiwa hilo bila ya kujua wabunifu wetu wanatengeza mavazi gani, wanashauri nini kikivaliwa na nini ndio mtu hupendeza, hawa si wabunifu tu bali ni washauri juu ya namna ya mavazi.” Alimalizia Robert.
Onesho hilo kubwa lilifanyika kwa siku tatu mfululizo liliteka jiji la Dar es Salaam huku ikishuhudiwa wanamitindo mbali mbali ndani na nje ya nchi wakionesha mavazi ya jukwaani lilivuta hisia za mashabiki wengi wa tasnia hiyo nchini.

إرسال تعليق