Mahusino
ya Diamond na Wema yameonekana kurudi kwa kasi hasa baada ya party
iliyofanyika December 25 pale Leaders iliyowahusisha watoto mbalimbali
kusherehekea Xmass na watoto wenzao ndipo kulipoonesha kuchipua upya kwa
mahusiano hayo.
Katika siku hiyo ya Xmass wakati Diamond akitaka kuanza kuimba wimbo
wake wa Ukimuona alimkatisha Dj na kuwauliza watoto’mimi mchumba wangu
nani?’watoto wakawa wanajibu Wemaaa,Ndipo Diamond akawatangazia watoto
kuwa ngoja aje mchumba wake wamuone alipopanda jukwaani alikua ni Wema
Sepetu.
Watoto walishangilia kuona hivyo sasa pengine walifurahi kuona
walichokua wakikitabiri ni sawa ama walifurahia kuona mahusiano juu ya
hao mastar wawili wa Tanzania yanaendelea,siku za hivi karibuni bado
watu wengi wamekua wakiendelea kuzungumzia uhusiano huo mmoja wapo
aliyeamua kupost mpaka kwenye akaunti yake ya Instagram ni mume wa
H.baba bibie Florah Mvungi.
Florah alipost picha inayomuonyesha Diamond akiwa kwenye pozi la
kimahaba na Wema huku chini akiandika ‘me na mume wangu tunapendana sana
but still tunaipenda sana hii couple iendelee kuwepo.Mungu awajalie
mapenzi tele wafike malengo all the best darlings.


إرسال تعليق