Hitmaker wa Mrs Super Star, Young Killer anapenda kurudi shule lakini tatizo hawezi kujilipia ada!!! Really???
“Mipango bado haijawa level,nilikuwa na plan niingie mwezi wa kwanza
,lakini kiukweli mambo hayajakaa vizuri,mambo ya ada nini
nakusanyakusanya bado,” rapper huyo alikiambia kipindi cha XXL cha
Clouds FM jana.
“Kuna sehemu pana chuo hapa Kinondoni na IFM kote nilikuwa na
plan,kiukweli ada bado haijakaa vizuri,kiukweli kwa mtu yoyote ambaye
ana uwezo wa kuniendeleza kimasomo mimi nipo tayari, kwasababu sasa hivi
na nia kabisa ya kusoma,kwasababu kilichonifanya nifeli ni kwasababu ya
muziki sasa muziki kiukweli nimeshafanya vizuri ,sasa nilikuwa nahitaji
kurudi shule. So kwa Mtanzania yoyote anayeweza kuniendeleza kielimu
mimi nipo tayari ninamwahidi nitasoma kwa bidii. Mtu yoyote ambaye ana
uwezo wa kunisomesha ajitokeze. Nataka kusomea IT. Course inagharimu
kama laki nane hivi.”
Young Killer amesema pesa alizokusanya mwaka jana katika shows zake, amezitumia katika kumjengea nyumba mama yake.
“Nilikuwa na plan kwasababu,nilikuwa na jenga nyumbani kwa bimkubwa
wangu,so nilikuwa naamini nitafanikiwa, lakini ujue hatuwezi kujua vitu
ambavyo vitakuja kujitokea mbele. So sasa hivi nina nia halafu ndio
mambo yamekuwa kama hayaeleweki hivi.”

إرسال تعليق