
Chelsea wameishinda Liverpool katika mbio za kumsaini winga
Mohamed Salah kutoka FC Basle kwa ada ya uhamisho ya £11million, hii ni
kwa mujibu wa mtandao wa klabu ya Chelsea.
Salah ambaye alikuwa anakaribia kujiunga na Liverpool,
lakini huku Juan Mata akiondoka darajani kwenda Old Trafford, Jose
Mourinho akaamua kutumia kiasi cha paundi millioni 37 kuwashinda majogoo
wa jiji.
Mchezaji huyo ambaye anaichezea timu ya taifa ya Misri
inaaminika alikuwa akipendelea kujiunga na Liverpool akiamini kwamba
atapata muda mrefu wa kucheza, lakini misuli minene ya fedha ya Chelsea,
pia na nguvu kubwa ya ushawishi ya Jose Mourinho – ikamfanya Salah
kubadili mawazo.
Chelsea wamethibitisha
kupitia mtandao wao leo jioni: ‘Makubaliano yamefikiwa baina ya FC Basel
kwa ajili ya uhamisho wa kiungo mwenye umri miaka 21 Mohamed Salah.
‘Uhamisho sasa unategemea kukamilika pindi Mmisri huyo atakapokubaliana na klabu maslahi binafsi na kufaulu vipimo vya afya.’
Salah baadae alitweet: ‘Mohamed Salah Officially in @chelseafc.’
إرسال تعليق