
Mchana wa leo katika dimba la Santiago Bernabeu mwanasoka bora wa
dunia, Cristiano Ronaldo aliionyesha kwa mara ya kwanza tuzo yake ya
Ballon D’or kwa mashabiki zaidi ya 80,000 waliojazana katika uwanja wa
nyumbani wa Real Madrid.
Ronaldo alishinda tuzo hiyo akiwapiku Lionel Messi na Frank Ribery ambaye alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kushinda pia.

Mashabiki wa Real Madrid walichora alama ya jina la Ronaldo kuonyesha mapenzi yao kwa mchezaji wao.

Gwiji wa klabu hiyo Alfred Di Stefano alikuwa mmoja ya watu waliokuja kumpongeza Ronaldo kwa kutwaa Ballon d’OR
إرسال تعليق