Na Andrew Chale, Zanzibar
MAKAMO Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambaye pia ni
Rais wa Serikali ya Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein kesho Januari
26, anatajiwa kumnadi mgombea wa Uwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki,
Mahmoud Thabit Kombo, katika uchaguzi mdogo unaoendelea kwenye jimbo
hilo.
Katika tarifa yake, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai
alisema kuwa, Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk Shein atakuwa mgeni
rasmi kwenye mkutano huo wa nne wa hadhara kwenye kampeni hizo
zinazoendelea.
Na kuongeza kuwa, Dk. Shein atawahutubia wananchi sambamba na kumnadi,
Mgombea huyo wa nafasi ya uwakilishi, Mahmoud Thabit Kombo, anayewania
nafasi hiyo kwenye jimbo hilo la Kiembesamaki.
Vuai aliwataka wananchi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi ilikusikiliza
sera na ilani za chama hicho katika utekelezaji wake iliwakichague
chama cha Mapinduzi kwa misingi imara ya kuwaletea maendeleo.
Aidha, kwa upande wake, Mahmoud Thabit Kombo aliwaomba wananchi wa
jimbo hilo, kumpigia kura hiyo Februari mbili, ili akawawakilishe kwenye
Baraza la Wawakilishi.
“Nawaomba Wanakiembesamaki, kutumia fursa ya kipekee ya kunichagua
ilikuweza kuwawakilisha kwenye BAraza, hakika chama chetu ni sikivu na
daima kipo na wananchi katika kuwatetea na kuwaletea maendeleo” alisema,
Mahmoud.
Kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Kiembesamaki, zilianza Januari 21,
ambapo zinatarajia kumalizika Februari Mosi, mwaka huu huku wananchi
wakitarajia kupiga kura ya chaguzi huo, Februari mbili.
إرسال تعليق