Muimbaji wa Kenya, Jaguar amesema mali alizokuwa nazo zimetokana na juhudi zake katika muziki pamoja na biashara halali.
Jagua alikuwa akizungumza kwenye kipindi cha na Strictly Kenya cha East Africa Radio jana.
“Unajua nilifanya nyimbo mpya inaitwa ‘Kioo’ kitu cha kwanza
kilinifanya nifanye huo wimbo yaani nikifungua Facebook watu wananiambia
sijui ‘upo kilo ngapi’,mimi mwenyewe sijui hata madawa zinakaaje. I
think yaani ni maombi mazuri,lakini mimi kwangu nafanya clean business
yaani sifanyi vitu vya kichini chini, mimi siuzi dawa,” alisema.
“Unajua muziki kama mimi siwezi sema nafanya muziki full time
kiukweli, lakini kwanza kitu cha kwanza, nimekuwa kwa game kama miaka
10,kwasababu watu wengine wanajua nimeanza juzi,lakini kama miaka 4.
After kufanya miaka 4 niliona ‘eeeh bhana nafanya show zote zile pesa
zinaisha’,that’s why nikaanza kujiinvest kidogo kidogo hivyo. Nilianza
tu na movie shop,yaani ile ya kukodisha zile,yaani kidogo kidogo naanza
taratibu business, naenda hivyo hivyo nafungua show room yangu ya
magari,kidogo kidogo hivyo yaani ilinionyesha nilianza kutumia jina
Jaguar kufika mbali,that’s why siku hizi unaniona na donate kutumia pesa
zangu ni kwasababu nimepitia maisha hayo. Nimefukuzwa sana shule
kwasababu ya karo ya shule. Ndio maana naamini hapa nilipofika ni watu
walinifikisha. Kwahiyi kusaidia mtu sio kwasababu nauza dawa na mimi
nilisaidiwa na watu mpaka kufika hapa,” aliongeza.
Akiongelea wimbo wake mpya, Kioo, Jaguar amesema alienda kwenye
gereza la ukweli kuomba afanye video yake na alipokelewa kwa mikono
miwili.
“Mimi sijionagi kama Jaguar kwasababu na believe binadamu wote tupo
sawa,” alisema. “Siku ya kwanza naenda kuangalia maandalizi za jela
,walifurahia sana yaani ni kama napiga show, ‘Jaguar! Jaguar!
wananiuliza wengi, walikuwa wanajua na mimi nimeshikwa kwasababu
nimeingia tu,wanajua nimeingia tu ili niletewe uniform, nikawaambia
‘wazee nataka kushoot video hapa’ ,hawakuamini kwasababu wana,believe
kuna klabu nzuri, nina magari mazuri. Nikawaambia ‘nataka kushoot video
na nyinyi, kwasababu mimi naamini kila binadamu ana makosa’. Kwahiyo
wale wako ndani sio kumaanisha wao ni watundu. Hakuna mtu hajawai
fanya makosa. Kwahiyo nilitaka kuonyesha hakuna mtu hakuwahi fanya
makosa, so nilikuwa nataka kuwaonyesha tupo pamoja na hata wakitoka
wanaweza fanya kitu cha maana, kwasababu ukiangalia wameweza fanya kitu
cha maana kama maactors na hakuna mtu tumeingia naye pale, wote
wameshikwa.Kama sasa hivi nilikuwa na mwambia rais wetu,yaani vijana
wako willing kufanya kazi,wakionyeshwa kama nikuact kama ni kuimba,
mpaka nikaona nijitolee nitoe kadhaa.
Post a Comment