RASMI JUAN MATA MCHEZAJI HALALI WA MANCHESTER UNITED, AFUZU VIPIMO VYA AFYA


Done deal: Mata signs for Manchester United for a club-record £37.1million from Chelsea
MANCHESTER United imetangaza rasmi kumsajili Juan Mata kutoka Chelsea kwa ada ya pauni milioni 37.1 mara baada ya kufuzu vipimo vya afya siku ya Jumamosi.
Kiungo huyo wa Hispania aliwasili kwenye uwanja wa mazoezi wa Manchester United (Carrington) kwa helkopta mapema Jumamosi  kabla ya kwenda kufanya vipimo vya afya.

Baadae United ikatupia picha ikimuonyesha Mata akiwa ametinga fulana ya klabu sambamba na kocha David Moyes wakati wa kusani mkataba.
Mata sasa anaweza kucheza mchezo wake wa kwanza siku ya Jumanne dhidi ya Cardiff City.

Post a Comment

Previous Post Next Post