Sandro Rosell Ajiuzulu Uraisi Wa Klabu Ya FC Barcelona…

SANDRO
Maswali mengi yamekuwa yakiamshwa kuhusu usajili halali wa mchezaji wa kikosi cha Barcelona, Neymar…Kupitia ukurasa wa Twitter wa mtandao unaotoa maelezo kuhusu matukio ya soka, ESPNFC, ulieleza uamuzi uliofikiwa na Sandro kuachia ngazi
ESPN

Pia, Rosell alieleza kufikia maamuzi hayo kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Twitter wa klabu hiyo ya Barcelona na kusema:
BARCA

Sakata hili linapelekea utafiti dhidi ya tuhuma kama mchezaji huyu, Neymar alisajiliwa kwenye klabu ya Barcelona kwa njia halali ama La. Neymar, alijiunga na timu ya Barcelona mapema msimu wa 2013-14. Utofauti kati ya kiasi cha pesa ambacho klabu hiyo ilitoa kumsajili mchezaji huyo na kiasi ambacho klabu alikotoka kimepokea, imeleta utata na kupelekea uchunguzi kwa tuhuma za ufujaji wa pesa ndani ya klabu hiyo.
Uamuzi wa Rosell kuachia ngazi umeleta maswali mengi dhidi ya tuhuma hizo endapo zina ukweli ndani yake, ila maamuzi ya mwisho ambayo yataandamana na ushahidi yatatolewa na mahakama.
Barcelona wamefanikiwa kupambana na kuongoza ligi ya Hispania, “La Liga”  na kuwa vinara kwenye ligi hiyo. Neymar, bila shaka amekuwa msaada mkubwa sana kwenye mafanikio haya
Neymar

Post a Comment

أحدث أقدم