
Wengi wa waandamanaji wanapinga nchi hiyo kujiunga na Muungano wa Ulaya
Ghasia zimeendelea katika mji
mkuu wa Ukrain,Kiev masaa machache baada ya Rais wa taifa hilo Victor
Yanukovych kutangaza kuwa analifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri
mbali na kuafikia makubaliano mengine ili kumaliza mzozo unaolikumba
taifa lake.
Mwandishi wa BBC mjini Kiev amesema kuwa aliona moto mkubwa katikati ya mji huo huku waandamanaji wakichoma matairi.Waandamanaji waliwarushia polisi fataki ,mawe na mabomu ya moto huku polisi nao wakijibu kwa kuwarushia mabomu ya kutoa machozi.
Awali Vitaly Klitchko ambaye ni mmoja wa viongozi wa upinzani alitoa wito kwa rais Yanukovych kujiuzulu kama njia pekee ya kusitisha maandamano hayo ambayo yameenea katika taifa zima la Ukrain.
إرسال تعليق