![]() |
Upinzani nchini Ukraine umetoa saa ishirini na nne kwa utawala wa nchi hiyo kuitisha uchaguzi mkuu, ama nchi hiyo ijiandae kwa maandamano makubwa zaidi.
Tangazo
la upinzani limetolewa wakati huu kukiripotiwa maandamano zaidi mjini
Kiev ambapo watu watano wameripotiwa kuuawa kwa kupigwa risasi wakati
wakikabiliana na polisi wa kutuliza ghasia.
Hapo jana
serikali ya nchi hio ilianza utekelezaji wa sheria yake inayokataza
maandamano kwenye sehemu za umma sheria ambayo imewafanya waandamanaji
kuwa wagumu zaidi kuondoka kwenye maeneo ambayo wanayakalia kwa sasa.
Waziri
mkuu wa taifa hilo, amesisitiza kuwa kile kinanchofanywa na upinzani
kinaenda kinyume na matakwa ya katiba ya nchi hiyo ingawa amekiri kuwa
serikali yake huenda ikatekeleza matakwa ya upinzani kuitisha uchaguzi
mwingine.
Rais wa
Ukraine Viktor Ianoukovitch aliwatolea wito wananchi wake jana
kutoshirikiana na wabaguzi wanaochochea machafuko katika mji mkuu wa
taifa hilo wa Kiev yaliosababisha vifo vya watu zaidi ya wanne.

Post a Comment