Viwanda vya Ngozi, Mafuta vyakamilika Shinyanga

viwandani 156
Kiwanda cha ngozi kilichopo manispaa ya Shinyanga ambacho kimekamilika na kazi ya kujaribisha mitambo inaendelea.
viwandani 159
Mkuu wa Mkoa Mhe. Ally N.Rufunga akipata maelezo ya maendeleo ya kiwanda hicho alipotembelea ili kuona shughuli zinazoendelea.
viwandani 163
Mashine za kuosha na kulainisha ngozi zikijaribiwa, chini ni ngozi zinazosubiri kuwekwa kwenye mashine hizo.
viwandani 165
Mkuu wa Mkoa akioneshwa baada ya kazi ngozi laini inavyokuwa na tayari kwa matumizi mbalimbali kama kutengeneza viatu,mabegi,pochi,n.k
viwandani 171
Hizi ni mashine za kutengeneza yuzi katika kiwanda cha nyuzi na nguo kilichopo manispaa ya Shinyanga.
viwandani 180
Mkuu wa Mkoa Mhe. Ally N. Rufunga akiona shughuli ya kujaribu mitambo katika kiwanda cha kukamua mafuta cha Jielong leo alipotembelea kiwanda hicho.
viwandani 181
Ndani ya kiwanda cha kukamua mafuta cha Jielong ambapo Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe.Ally N. Rufunga amekitembelea mapema leo na kujionea kazi ya kujaribu mitambo.
Kiwanda cha kutengeneza Ngozi kwa ajili ya matumizi mbalimbali cha kampuni ya Kichina “Xiu hua”  kilichopo katika Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga kimekamilika ambapo mhandisi na msimamizi wa kiwanda hicho “Mr.Way” amesema kwa sasa majaribio yanafanyika kabla ya kuanza uzalishaji wakati wowote.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Ally N.Rufunga ametembelea kiwanda hicho mapema leo na kujionea majaribio ya mitambo ya kutengeneza ngozi za mbuzi,kondoo na ng’ombe.
Kiwanda hicho kinachotarajiwa kutengeneza jumla ya ngozi za kondoo na mbuzi Elfu kumi hadi 12 kwa siku na ngozi za ng’ombe 2500, kitaajiri zaidi ya Watanzania 500 ambapo Mr.Way amesema kipaumbele zaidi ni kwa wakazi wa mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa pia ametembelea kiwanda cha kukamua mafuta ya pamba cha Jielong Holdings, ameelezwa na Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda hicho Mr. Jerry Q kuwa wanaendelea kuzifanyia majaribio mashine na wakati wowote kitaanza kazi ya uzalishaji.
Mr.Jerry amesema kitaajiri zaidi ya wananchi 180 kitakapoanza uzalishaji na tayari kimeanza kuajiri.
Aidha,kiwanda cha kutengeneza nyuzi za nguo cha Dahong ambacho  kinatarajiwa kuanza kazi mapema mwezi Machi baada ya kukamilisha kazi ya kufunga mashine mwishoni mwa mwezi Februari.
Msimamizi wa kiwanda hicho Mr.Saimon amesema kiwanda hicho kitaajiri wananchi zaidi ya 80.
Mhe.Rufunga amefanya ziara hiyo ili kujua maendeleo ya viwanda hivyo ambavyo vinatarajiwa vitakapokamilika pamoja na viwanda vingine, vitabadili sura ya mkoa wa Shinyanga kimaendeleo kwa kukuza uchumi wa mkoa,kwani amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha maisha ya wananchi wa Shinyanga yanabadilika kwa kuhamasisha uwekezaji katika viwanda vitakavyozalisha ajira nyingi zitakazonufaisha wananchi.

Post a Comment

Previous Post Next Post