Mara nyingi huwa vigumu kwa rapper mkubwa wa Tanzania
kukubali kuwa alirap kwa kufuata mtindo wa rapper mwenzake wa hapa
Tanzania na mwisho kuingiza pesa hata zaidi ya aliyemuiga. Wengi
watakwambia mimi namfuatilia sana Jay-Z, Lil Wayne na wengine.
Hiyo imekuwa tofauti kwa baba yake Qayllah, Shetta ambaye amekiri
kuwa alitumia mtindo wa rapper wa Choka Mbaya, Black Rhino na akapita
‘mulemule’.
Shetta amefunguka katika mahojiano aliyofanya na Jabir Saleh aka
Kuvichaka kupitia The Jump Off ya 100.5 Times Fm akiwa kama mkali wa The
Jump Off wa wiki.
“Umenikumbusha, Rhino pia ni mtu niliyekuwa namsikiliza, Rhino na
Noorah sana. Ndio maana ukisikiliza nyimbo yangu ya kwanza nimefanya
kama Rhino.” Amesema Shetta.
Mkali huyo wa Nidanganye alirap kidogo kuonesha kweli alipita
mulemule kwa Rhino, “Hizo ‘sawaa’ nini zote zilikuwa vitu vya Rhino
alikuwa anapenda kupita.”
Hata hivyo, Shetta alipoambiwa amemkopi kabisa Rhino na kuwa Rhino
mwingine, ilimbidi atafute jinsi ya kuweka vitu vyake ili awe yeye.
“Nilikuwa namfeel, sasa baada ya kutoa ngoma ile watu wakasema ‘Rhino
mtupu’ kwa hiyo nikawa najaribu ku-create kitu changu kingine, kwa
sababu kweli ukisikiliza unasema yeah huyu Rhino huyu.”
Katika hatua nyingine, Shetta aliiambia Tovuti ya Times Fm kuwa hivi
sasa anaingiza zaidi ya milioni 5 kwa kila show na amewahi kuvunja
rekodi ya ukumbi wa Bilicanas kwa kujaza watu.
“Sasa hivi nimepandapanda kidogo, kuanzia sita M, nafanya…sita au
tano. Muziki umebadilika kwa sababu sasa hivi watu wanaingiza hela. Kwa
hiyo nasisitiza tunaangalia na ukubwa wa show, na nani kaja. Kuna
rappers, lakini wanarap vipi? Katika midundo gani, muziki wao upo katika
career gani? Mimi ni mfanyabiashara. Mimi nahisi kwenye ule ukumbi wa
Bilicanas hakuna mtu ambaye amevunja rekodi kwa kujaza watu kwenye show.
Kama mimi show yangu ya mwisho wenyewe walikuwa wanakiri. Show
zinatokea zinaenda zinarudi lakini mimi nilivunja kwa sababu tiketi
ziliisha watu walikuwa nje wanataka kuingia lakini wakawa hawaruhusu
tena watu.
“Nina fans wengi, muziki wangu unaniruhusu kufanya hivyo. Rappers
wengi wanaimba muziki ambao yaani ile kibiashara hauko sawa. Kwa hiyo
wakija kwenye biashara sawa. Tunaweza tukasikia kuna mtu nae katangaza
hivyo.”
إرسال تعليق