Baada ya kuvuna mafanikio kadhaa kupitia muziki wake ikiwa ni
pamoja na kuzoa tuzo hapa nyumbani, na video yake ya ‘Jikubali’ kuwa ya
kwanza kuchezwa Channel O, mwimbaji wa ‘Unanichora’ Ben Pol amepata
shavu la kwenda nchini Ujerumani kufanya show mwisho wa mwezi huu.
‘Team Ben Pol is gonna be perfoming in München on 30th April 2014 #Twendesasa #Ready???’, hiyo ni status ya Ben Pol kupitia ukurasa wake wa Facebook.

Ben Pol ambaye ameachia album yake mpya siku chache zilizopita
online, amesema kuwa show hiyo ya Ujerumani ndio ya kwanza ya
kimataifa kuwahi kuipata, japo atakapokuwa huko anatarajia kufanya show
zingine katika miji iliyoko karibu na anakoenda japo kwasasa hiyo ya
Munchen ndiyo iliyothibitishwa.
Ameongeza kuwa waandaaji wa show hiyo walimtafuta takribani miezi
mitatu iliyopita na wakawa bado hawajafikia makubaliano hadi kipindi
hiki.
إرسال تعليق