
Baadhi ya wanafunzi nchini Nigeria
JESHI la Polisi Nchini Nigeria limesema kuwa Shule ya bweni ya Wasichana imeshambuliwa katika Jimbo la Borno Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo huku baadhi ya wasichana wakitekwa nyara. Wazazi wanasema kuwa zaidi ya wasichana miambili wametekwa nyara na washambuliaji hao. Kwa mujibu wa taarifa zinazohusiana na siasa nchini humo zinasema washambuliaji hao wanaaminika kuwa ni wanachama wa kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Boko Haram.
Utekaji nyara huo ulifanyika usiku wa manane katika shule ya Chibok
ksuini mwa mji wa Borno, karibu na mpaka na Cameroon. Inaarifiwa
wasichana 300 walikuwa wanajiandaa kwa mitihani yao. Mmoja wa wasichana
alifanikiwa kutoroka na aliambia BBC kuwa walikuwa wanalala wakati
walipovamiwa na wanaume waliokuwa wamejihami. Waliowashambulia
wanaaminika kuwa wapiganaji wa kundi la Boko Haram.
Wanaume hao waliingiza magunia ya chakula katika malori yaona
kuwaamuru wasichana kuyapanda malori hayo. Wasichana 15 walifanikiwa
kutoroka baada ya lori walimokuwa kukumbwa na hitilafu. Wakazi wa kijiji
cha Chibok wanasema kuwa walisikia milipuko kadhaa huku nyumba 170
zikiteketezwa.
Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa wanajeshi wawili
waliuawa huku mali ikiharibiwa wakati wa shamblizi hilo mjini Chibok.
Mnamo siku ya Jumatatu, zaidi ya watu 70, waliuawa katika milipuko
miwili ya mabomu katika kituo cha mabasi mjini Abuja. Kundi la Boko
Haram pia limelaumiwa kwa kufanya shambulizi hilo.
-BBC
Post a Comment