Homa ya kidinga popo yasambaa Tanzania, mmoja athibitika kufariki.

Mbu anayeambukiza kidinga popo
Nchini Tanzania watu 147 wamethibitika kuwambukizwa ugonjwa wa homa ya kidinga popo yaani homa ya dengu huku mtu mmoja akiripotiwa kufariki dunia kwa ugonjwa huo.
Kasi ya ugonjwa huo ambao ikiwa hautadhibitiwa unaweza kuleta madhara dalili zake zinashabihiana na zile za malaria kwani unaambukizwa kwa kupitia mbu na unadaiwa kusambaa katika maeneo mengine nchini Tanzania ingawa kwa sasa uko zaidi mjini Dare salaam.
Taarifa zinasema kuwa kuna visa vya wagonjwa nchi jirani ya Msumbiji taifa linalopakana na mkoa wa Mtwara jambo linalozua wasiwasi wa kuwa na visa vingine mkoani humo. Kutaka kufahamu hatua zinazochukuliwa na serikali ya Tanzania Joseph Msami amezungumza na Dk Janet Mgamba ni kaimu mkurugenzi msaidizi wa udhibiti na ufuatailiaji wa magonjwa ya milipuko ambaye anaanza kwa kueleza hali ya kidinga popo ilivyo.
(SAUTI MAHOJIANO)

Post a Comment

Previous Post Next Post