Baada
ya sakata la msanii wa Hip Hop wa siku nyingi hapa nchini kwa tuhuma za
kumkata sikio mama yake mkubwa huko mjini Mwanza leo limechukua sura
nyingine baada ya mtangazaji wa kipindi cha Amplifaya cha siku ya Leo
muda mchache uliopita kurusha taarifa kuhusiana na tuhuma hizo. Dudu
Baya ambae alikanusha kwenye simu kuwa yeye hajafanya kitendo hicho cha
kinyama na alikua Shinyanga kwenye shughuli zake na kusema kuwa hao
ndugu zao hawana hata mawasiliano nao mazuri lakini ni tofauti kabisa na
maneno ambayo ameongea bibi huyo.
Akiongea kwenye kipindi cha AMPLIFAYA
cha mtangazaji Millard Ayo ndani ya Clouds FM bibi huyo alisema kuwa
majira ya jioni Dudu Baya alifika nyumbani hapo na yeye alimkaribisha
ndani na baada ya kuketi alianza kumuuliza maswali kuwa kwanini
anawaroga wadogo zake na yeye alikanusha swala hilo na Dudu Baya
alichukua kisu na kumkata sikio na kiasi cha kumsababishia maumivu
makali sana Mama huyo. Shahidi mwingine ambae amethibitisha tukio hilo
ni kijana ambae ameongea kuwa yeye anamuita DUDU BAYA baba mdogo kuwa,
ni kweli kitendo hicho kilitokea na wao walimchukua bibi huyo na
kumpeleka polisi kupata PF3 na kumpeleka bibi huyo hospitali kwa
matibabu.
Hichi ni kitendo cha kinyama sana
alichotendewa Bibi huyu na ukizingatia ni mwanamke ambaye hana nguvu za
kiweza kumuhimili kipande cha baba mtu mzima kama Dudu Baya. Serikali
lazima iangalie kwa makini swala hili na sio kuleta maneno ya ajabu kama
aliotamka dudu baya akihojiwa kwenye radio kuwa “Mimi Polisi wote wa mwanza wananijua na namba zangu za simu wanazo”,
swala hili sio la kirafiki au la kukejeri kwenye vyombo vya habari na
hasa Jeshi la Polisi kuweza kuchekea maneno ya uongo anayoweza kuongea
kwenye vyombo vya habari bila kuchukuliwa hatua za kisheria. WANAWAKE na
bila kusahau VYAMA vya wakina MAMA nchini kote hii ndio nafasi “Fursa”
ya kuweza kutumia msanii huyu kuwa mfano wa kuweza kuogopesha wengine
wengi wenye unyanyasaji huu wa mwanamke mpaka kufikia kufanya na mtu
ambae ni msanii na anaangaliwa kama kioo cha jamii, amepata nafasi ya
kuwa kioo cha jamii ameshindwa kuitumikia hiyo na ameamua kuwa na tabia
za kipumbavu katika jamii.
PICHA: Kwa hisani ya “millardayo.com”
Post a Comment