Katibu
Mkuu wa CCM,Kinana akiwa na viongozi wengene wakiangalia jinsi
watanzania wanavyopata taabu na kunusurika kifo kwa kuvuka kwenye Mto
Malagalasi wakitokea kuuza bidhaa zao na kununua mahitaji mengine katika
Soko Buhinja, Kijiji cha Mrambi, Mkoa wa Makamba nchini Burundi.
Wananchi hao kutoka Kijiji cha Kibande na vijiji viongine wilayani
Buhigwe, Kigoma Tanzania, huenda Burundi kufanya biashara kutokana na
upande wa Tanzania kutokuwepo na soko kunakosababishwa na kodi nyingi.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiangalia mto Malagalasi ambao ni
mpaka wa Tanzania na Burundi, alipokuwa katika ziara wilayani Buhigwe
mkoani Kigoma,Kinana yupo katika ziara ya siku 5 mkoani humo ya
kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa
kwa kufuata Ilani ya CCM.
Hizi
ni baadhi ya picha zinazoonesha jinsi wananchi wa Tanzania wakivuka mto
huo na wengine kuvushwa kwa malipo, wakirudi Tanzania baada ya kufanya
biashara upande wa Burundi.
Watu
wote hao wakisubiri kuvushwa kwenye mto huo Malagalasi,kwa kimtumbwi
kimoja ama kubebwa kama baadhi ya picha zinavyoonyesha
Baadhi
ya Wanahabari pichani Kulia Bakari Kimwanga kutoka gazeti la Mtanzania
na Bwana Jongo kutoka gazeti la Uhuru wakionja joto ya kuvushwa kwenye
mto wa Malagalasi ambao ndio sehemu ya mpaka kati ya Burundi na
Tanzania.Kuonja adha hiyo hulipia kiasi cha fedha shilingi 500 mpaka
1000 kama nauli.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza jambo kwa msisitizo na Mkurugenzi
wa Maendeleo wa Halmashauri ya Buhigwe,Kaondo Julius walipokwenda
kukagua mpaka wa Tanzania na Burundi alipokuwa katika ziara wilayani Buhigwe mkoani Kigoma.
Mbunge wa
Jimbo la Manyovu wilaya ya Buhingwe,Mh.Albert Obama Ntabaliba
akizungumza na Wanakijiji cha Kibande,kwenye mkutano wa hadhara wilayani
Buhigwe mkoani Kigoma
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha
Kibande,kwenye mkutano wa hadhara wilayani Buhigwe mkoani Kigoma
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa chama cha
CNDD-FDD,Mkoa wa Makamba nchini Burundi,Bwa.Nishimwe Zen,kabla ya
mkutano wa hadhara kufanyika katika kijiji cha Kibande,wilayani Buhigwe
mkoani Kigoma.
Wanachama waliohamia chama cha CCM wakionesha kadi zao ambazo walimkabidhi Katibu Mkuu wa CCM,na kukabidhiwa kadi mpya za CCM.
Sehemu ya
Wanachama wapya waliojiunga na CCM,wapatao zaidi ya 300 wakila
kiapomara baada ya mkutano wa hadhara kufanyika katika kijiji cha
Kibande,wilayani Buhigwe mkoani Kigoma.
Baadhi ya Wakazi wa kijiji cha Mnanila-Manyovu wakishangilia jambo wakati katibu MKuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowahutubia
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia baadhi ya Wakazi wa kijiji cha Mnanila-Manyovu
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Mnanila-Manyovu .
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Kamati ya Siasa Wilaya ya Buhingwe na kupata taarifa mbalimbali za maendeleo.
Mkurugenzi
wa Maendeleo wa Halmashauri ya Buhigwe,Kaondo Julius pamoja na Afisa
Mipango,Charles Mduma wakitoa ufafanuzi mfupi kwa Waandishi wa habari
kuhusiana na taarifa ya Maendeleo ya Wilya ya Buhingwe iliyotolewa kwa
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa
Manyovu-Wilaya ya Buhigwe.Mh Albert Obama,mara baada ya kumaliza kikao
cha siasa cha wilaya
Baadhi ya Wakazi wa Buhigwe wakimpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowasili wilayani humo mkoani Kigoma.
Ndugu Kinana akizungumza jambo na baadhi ya Wananchi wa Buhingwe huku wakimsilikiza kwa makini.CHANZO MICHUZIJR
Post a Comment