Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC) ikiwa katika ukumbi wa Bunge mjini
Dodoma mara baada ya timu hiyo na viongozi wao kutembelea Bunge Maalum
la Katiba leo.
Keptain Msaidizi wa Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC) Frank William
akipeana mkono na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali
Iddi mjini Dodoma mara baada ya timu hiyo na viongozi wao kutembelea
Bunge Maalum la Katiba leo .
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara
pamoja na Naibu wake Juma Nkamia wakiwa wameshikilia Kombe la ushindi
la Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC)baada ya timu hiyo kutembelea Bunge
Maalum la Katiba mjini Dodoma leo.
Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC) ambao ni Bingwa wa Dunia kwa mpira wa
miguu kwa watoto wa mitaani wakiwasili nyumbani kwa Waziri Mkuu leo
mjini Dodoma mara baada kutembelea Bunge Maalum la Katiba .
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akipokea kutoka kwa nahodha msadidizi wa timu ya
soka ya Tanzania ya Watoto wa Mitaani, Frank William, kombe la ubingwa
wa dunia wa soka la watoto wa Mitaani wakati alipowaandalia chakula cha
mchana kwenye makazi yake mjini Dodoma Aprili 11,2014. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)Wachezaji
wa Timu ya Soka ya Tanzania ya Watoto wa Mitaani, waliotwaa ubingwa wa
Dunia wakipata Chakula cha mchana kilichoandaliwa na Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda kwa ajili yao kwenye makazi yake mjini Dodoma Aprili 11,
2014. (Picha na Ofiai ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Timu
ya Soka ya Tanzania ya Watoto wa Mitaani, waliotwaa ubingwa wa Dunia
katika Chakula cha mchana kilichoandaliwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
kwa ajili yao kwenye makazi yake mjini Dodoma Aprili 11, 2014. (Picha na
Ofiai ya Waziri Mkuu)
………………………………………………………………
Na Magreth Kinabo –Dodoma
Mfungaji bora wa Timu ya Watoto wa Mitaani kutoka Mwanza Tanzania,
(TSC)ambayo iliibuka mshindi katika mashindano Kombe la Dunia la Watoto
hao yaliyofanyika Brazil, mwaka huu Frank William ameishauri ,
Serikali na jamii kuwasaidia watoto wa mitaani ili kuweza kukuza vipaji
vyao.
Kauli hiyo ilitolewa leo mjini Dodoma na William wakati walipolitembelea
Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma , wakiwa na viongozi wao ,ambapo
walipata nafasi ya kuzungumza na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Dk. Fenella Mukangara pamoja na Naibu wake Juma Nkamia.
Alisema siri ya ushindi wetu ni ushirikiano na kujituma, tukilikwenda
kuwakilisha watoto wengine wa mitaani. Hivyo aliomba jamii kuwasaidia
watoto wengi wa mitaani ambao hawana uwezo wa kupata elimu lakini wana
vipaji mbalimbali ili waweze kuvikuza.
Kwa upande wake kipa bora wa timu hiyo, Emmanue Amos, alishauri Serikal
iweze kuwasaidia ili waweze kushiriki katika mashindano ya mwaka 2018
ya kombe hilo.
Mchezaji mwingine wa timu hiyo ,Denis David aishauri jamii isiwadharau
kwa kuwa ni watoto wa mitaani kwani wanavipaji wakipata watu wa
kuwasaidia, hivyo aliitaka iwekeze katika soka la vijana kwa sababu
baada ya miaka 20 ijayo mchezaji bora anapatikana kwa njia hiyo.
Aliwaomba wajumbe wa Bunge hilo ,kuwasaidia ili waweze kuvikuza vipaji vyao.
Naye Kocha wa timu hiyo,Suileiman Jabir alisema wadau mbalimbali
kuwasaidia na kuwaendeleza watoto hao I, ambao ni wengi ambao wanaweza
kuwa na vipaji vya sanaa na utamaduni.
Akizungumzia kuhusu mafanikio ya ushindi huo, ni kuwa na mpango wa
kutafuta vijana wenye vipaji ambapo wanaviendeleza na kuvikuza kwa
kufanya maandalizi ya kiutalaamu na kiufundi.
Jabir aliongeza kuwa waliwandaa kisaikolojia ili waweze kushinda katika mashindano hayo ya kimataifa.
Aliwataka wajumbe wa Bunge hilo, kuhakikisha was aula la watoto hao,
linapewa kipaumbele na kuweka sheria itakayowadhibiti wakina baba
wanatekeleza watoto,huku akiisa jamii kuwasaidia watoto pale wazazi au
walezi wanapofariki dunia.
Rais wa timu hiyo, Altaf Hirani aliiomba Serikali kuweza kuwasaidia
kupata kiwanja cha michezo kwa ajili ya watoto jijini Mwanza au kwenye
maeneo mengine ya nchi.
Credit:Shaffihdauda
Post a Comment