Madaktari nchini Marekani wamefanikiwa kuwatengezea wanawake wanne sehemu ya uke kwa njia ya kisayansi.
Walitumia mfano wa seli ya uke na
mifupa ya mwili kuweza kukuza uke huo katika maabara kwa kuzingatia
wastani na umbo la kila mwanamke.
Baada ya matibabu hayo, wanawake hao wote
inaarifiwa walielezea kupata hisia sawa na kamilifu,matamanio,
kuridhishwa wakati wa tendo la ndoa pamoja na kutopata maumivu yoyote
wakati wa tendo la ndoa.
Wataalamu walisema kuwa utafiti wao, ambao
matokeo yake yalichapishwa katika jarida la kisayansi la Lancet, ni
mfano wa hivi karibuni wa nguvu za mbinu tofauti na za kisasa za
matibabu.
Wanawake hao walizaliwa na uke ambao haukuwa
umeumbika vyema yaani ulikuwa na kasoro ya maumbile , tatizo
linalojulikana kama ‘vaginal aplasia.’
Matibabu ya kisasa kwa tatizo kama hilo la kiafya yanaweza kuhusisha upasuaji ambapo ngozi au sehemu ya utumbo inatumika.
Celi zilichukuliwa kutoka kwa kizazi cha kila
wanawake hao ambacho kilikuwa na kasoro ya maumbile na kukuzwa katika
maabara ili kuweza kuzaana.
Picha za kizazi cha wanawake hao zilitumia kuwarekebishia uke wao.
Hili bila shaka ni jambo geni katika sayansi ya matibabu na pia inatoa taswira ya mambo yatakavyokuwa katika siku za usoni.
Jambo la Kutumia celi za mwili kubadilisha
maisha ya wagonjwa tayari limefanyika na kuwasiaidia wagonjwa kupata
kibofu cha mkojo, mishipa ya damu na koo.
Sasa unaweza kuongeza kwenye orodha hiyo, uke na pua
- bbc
Post a Comment