Mkurugenzi wa Facebook wa Ushirikiano na Ukuaji wa Kimataifa, Bw. Nicola D’Elia akiongea katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Bw. Diego Gutierrez (kushoto).



---
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Kampuni 
ya simu ya mkononi TIGO  imetangaza kuingia katika ushirikiano na 
kampuni ya mtandao wa kijamii Facebook ambapo wateja wake wote nchini 
watapata huduma ya Facebook bure kwa lugha ya Kiingereza na kwa mara ya 
kwanza, katika lugha ya Kiswahili kupitia simu zao za mkononi.
Hii ni 
mara ya kwanza kwa Facebook kupatikana bila malipo kwa mtandao wowote 
eneo la Afrika mashariki, kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Diego 
Gutierrez.  
Akizungumza
 katika tafrija ya uzinduzi wa ushirikiano huo jijini Dar es Salaam, 
Gutierrez alisema: “Ushirikiano huu unamaanisha kwamba wateja wa Tigo 
kwa mara ya kwanza watakuwa na uwezo wakutumia Facebook kupitia simu zao
 za mkononi bila kukatwa gharama yeyote katika utumiaji wa data, hivyo 
kuwawezesha kuungana na watumiaji wapatao milioni 2 wa mtandao huo wa 
kijamii waliopo nchini Tanzania kati ya watumiaji bilioni 1.2 duniani 
kote.”
Gutierrez
 aliongeza: “Hii ni kwa mara ya kwanza mtandao wowote mkubwa wa kijamii 
umeweza kupatikanika kwa Kiswahili, lugha ya taifa inayotumika na 
Watanzania na wingi wa watu walio katika kanda ya Mashariki, Kati na 
Kusini mwa Afrika. ”
“Facebook
 imekuwa chachu kubwa ya utumiaji wa data kwa mitando ya simu. Kwa 
ushirikiano huu wa kipekee, Tigo imepewa kipaumbele kuliko mitandao 
mingine katika kuwaletea wateja wengi ladha mpya ya utumiaji waintaneti 
na mitandao ya kijamii kupitia lugha ya Kiswahili. Hii ndio maana halisi
 ya maisha ya kidigitali, pia inatimiza malengo yetu ya kuwashawishi 
wateja wengi zaidi wa Tigo kutumia data katika matumizi yao ya 
mawasiliano ya kila siku.”
Mkakati huu wa ushirikiano ni muendelezo wa mpango wa Facebook unaoitwa Internet.org uliozinduliwa na muasisi wa kampuni hiyo, Mark Zuckerberg.
Gutierrez
 alisema, “Huduma hii mpya itafungua milango mipya kwa Watanzania na 
watumiaji wengine wa Kiswahili kupata fursa za kibiashara, kielimu, na 
nyinginezo za kijamii na kiuchumi duniani kote.”
Ukiondoa 
nchi tano wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Kenya, 
Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi, Kiswahili pia kina zungumzwa katika
 maeneo ya Malawi, Somalia, Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na 
Msumbiji.
Kwa 
uzinduzi huu, Tanzania taifa linayojulikana kama chimbulo la lugha ya 
Kiswahili, inayofahari ya kuwa nchi ya kwanza katika ukanda huu 
kutangaza lugha hii kimataifa, mafanikio ambayo hatuna budi yanatokana 
na ushirikiano kati yaTigo, kampuni mama ya Millicom na Facebook.
Hii ni 
mara ya pili kwa kampuni ya Facebook na Millicom kushirikiana katika 
kuzindua huduma ya Facebook kupitia simu bure ambapo Tigo nchini 
Paraguay walizindua huduma hii kwa mara ya kwanza Desemba 2013 katika 
lugha ya kiguarani inayotumika nchini humo. 
Mkurugenzi
 wa Facebook wa Ushirikiano na Ukuaji wa Kimataifa Nicola D’Elia 
alisema, “Tunayo furaha kushirikiana na Tigo kwa mara nyingine tena kwa 
kuwapatia Watanzania wengi zaidi uwezo wa kuwasiliana kupitia utumiaji 
bure wa data katika app ya Facebook na tovuti ya simu, na sasa katika 
lugha ya Kiswahili.”
إرسال تعليق