Muigizaji wa filamu ya hadithi ya biblia, Noah, Russell Crowe
alihangaika mwezi March kutafuta mkutano ambao ungeonekena kama kuungwa
mkono (endorsement) kwa filamu hiyo na Papa Francis na Vatican. Kwa
mujibu wa gazeti la jana la Vatican liitwalo Avvenire, staa huyo
hakuweza kufanikiwa.
Gazeti hilo la Avvenire limeiita filamu ya Noah “fursa iliyopotea’,
na Nuhu bila Mungu. Liliendelea kuwa kuandika kuwa filamu imeuelezea
mkasa wa Nuhu na gharika kama nafasi iliyopotezwa. Crowe, muongozaji wa
filamu hiyo, Darren Aronofsky na mtayarishaji, Scott Franklin pamoja na
mwenyekiti wa kampuni ya Paramount, Rob Moore wote walisafari kwenda
Vatican, March 19.
Kwa ufupi timu hiyo ilikutana na kiongozi huyo wa kanisa katoliki
duniani aliyewabariki pamoja na watu wengine 40,000 kwenye kanisa la St.
Peter’s Square lakini filamu hiyo haikujadiliwa.
Filamu hiyo imepigwa marufuku kuoneshwa kwenye nchini nyingi za Kiislamui duniani.
Post a Comment