![]() |
H.Baba akiwa kwenye kaburi la Dandu |
Msanii wa muziki, H.Baba hivi karibuni alilitembelea kaburi la
mmoja wa waasisi wa tuzo za muziki za Tanzania, KTMA na msanii wa muziki
marehemu James Dandu aka Cool James.
Kupitia Instagram H.Baba ameandika: Nipo Ngudu Kwimba apo ndipo
alipopumzishwa shujaa wetu wa mwanza Cool James Dandu, Nilienda
kusafisha kabuli lake nakushirikiana na ndugu zake kiukweli nilipokelewa
vizuri sana nyumbani kwao nafamilia ya Dandu nikamuona na mzee Dandu
mwenyewe . Wasanii wenzangu muwe mnapita japo kwa shujaa wetu,kuna leo
na kesho nawewe haupo wasanii wenzio watakupotezea ata kama umetenda
mema kiasi gani? Jitambue kijana nimuda wako ila kumbuka kunakufa pia,
tukumbuke kusali nakumuomba mungu tunapokwenda atupajui?”Alisema H.Baba

H.Baba akiwa na wazazi wa marehemu Dandu

H.Baba akiwa na wazazi wa marehemu Dandu
Katika picha nyingine msanii huyo aliandika: Nawaasa wasanii wenzangu
mnaoshiriki tuzo za Kill Music Awards mkibahatika kupata tuzo hii yenye
heshima kubwa Tanzania ipelekeni kwa mtoto wa Dandu atafurahi sana japo
katutangulia mbele za haki,nawaombea kwa Watanzania wote wawapigie kura
wanamuziki wa mwanza kwenye Kill ili tupeleke tuzo kwa ndugu yetu kaka
yetu mwanamuziki mwenzetu alieitangaza Tanzania kimuziki Kimataifa
nakitaifa .. Mungu ibariki mza tufanikishe hili #mpigie kura @fidQ
@youngkillermsodoki ili tufikishe ushindi wetu pale kwa familia ya dandu
. #kwimba ngudu. Tunakaribisha ata kama msaanii mwingine akijitolea
kama msanii Kala Jeremah alivyofanya mwaka jana kwakupeleka tuzo kwa
mama yake na Mangwea, r.i.p Dandu, r.i.p Sharobalo, r.i.p Langa, r.i.p
Mr.Ebbo, r.i.p Stive2k, r.i.p Complex r.i.p Lady Luu r.i.p N.K … Sote
tupo njia moja tujiandae.”

H.Baba akifanya usafi kwenye kaburi la Dandu

H.Baba akiwa kwenye kaburi la marehemu Dandu na baadhi ya ndugu wa Dandu

إرسال تعليق