Taarifa juu ya ugomvi ulioibuka wiki iliyopita baina ya ndugu mapacha wa kundi la P-Square Peter na Paul
na kaka zao zimewashtua mashabiki wao walioko pande mbalimbali za
dunia. Chanzo kimoja cha karibu na ndugu hao kimeelezea sababu na kile
kilichotokea.
Inadaiwa kuwa ugomvi wa wanandugu wa familia ya Okoye ulianzia kwa wasaidizi wao binafsi, ‘Personal Assistants’ (PA’s).
Ripoti kutoka katika vyanzo mbalimbali vya Nigeria zinasema kuwa ‘PA’
wa kaka yao mkubwa Jude aitwaye Wande alimpatia ‘PA’ wa Peter aitwaye
Shege, pesa ili akamsajilie gari lake, lakini inasemekana ‘PA’ wa
Peter badala ya kutumia pesa hizo kwa kazi aliyoelekezwa alizitumia kwa
kitu tofauti.
Baada ya hapo inadaiwa kuwa ‘PA’ wa Jude alikasirika baada ya
kugundua kuwa pesa alizompa ‘PA’ wa Peter hazikufanyiwa kazi
aliyoelekeza. Alipoenda nyumbani kwa Okoye’s ‘Squareville’ ili
kukabiliana na ‘PA’ wa Peter ndipo ugomvi ulizuka baina ya wasaidizi
hao wawili wa ndugu.
Chanzo kinaendelea kusema baada ya ugomvi kuanza Peter aliingilia na
kutaka kumpiga msaidizi wa Jude hadi Paul alipoingilia kwa lengo la
kuwaachanisha, lakini badala yake Peter alijikuta akimpiga ngumi pacha
wake Paul na kuanguka chini japo inadaiwa kuwa Paul hakumrudishia ngumi
kaka yake, na badala yake kaka yao mwingine aitwaye Tony naye
aliingilia na kuanza kupigana na Peter. Wakati haya yote yanatokea mke
wa Paul Anita alikuwa akishuhudia.
Chanzo kiliongeza kuwa Peter anataka awe mhusika mkuu wa maswala ya
fedha za kundi au apate mgao mkubwa zaidi, huku upande wa pili inadaiwa
Paul anataka kaka yao mkubwa ambaye pia ni meneja wao Jude aendelee
kuwa msimamizi mkuu wa maswala ya fedha zao kama ilivyokuwa miaka yote
iliyopita, lakini mpaka ilifikia hatua ya kutaka wagawane mali kila mtu
awe na chake.
Baada ya habari za ugomvi baina ya wana ndugu hawa kuenea, hii ni
post ya Paul aliyoiandika juzi kupitia ukurasa wake wa Facebook.
“After the storm comes the calm. Hoping for better days ahead as one family. God’s intervention.”
إرسال تعليق