![]() |
| Mashine za kuuza bangi Marekani |
Baada ya Marekani kuhalalisha matumizi ya bangi katika baadhi ya
majimbo kama Colorado ambapo sasa ni ruksa kununua na kutumia kwa
matumizi binafsi na ya kitabibu (mediacl marijuana), sasa huduma hiyo
inapatikana katika mashine maalum huko Colorado.
Mashine hizo zinapatikana kwa dispensary zilizosajiliwa na zenye
leseni kwaajili ya kuuza marijuana kwa ajili ya matibabu, ambapo sasa
watumiaji wanauwezo wa kununua muda wowote moja kwa moja kwenye mashine
hizo tofauti na mwanzo ambapo iliwabidi kupanga foleni kaunta.

Akizungumza katika uzinduzi wa mashine hizo CEO wa kampuni
iliyozitengeneza Mr Stephen Shearin amesema, Ili mtumiaji aweze kununua
bangi katika mashine hizo atahitajika ku swipe kadi yake ya kitambulisho
ili mashine iweze kumtambua kama ndiye mmiliki wa kitambulisho hicho
kupitia kamera zilizofungwa.
“Swipe ID and get verified. Select products and pay. Retrieve products and depart using appropriate bagging solution.” Alisema.

Aliongeza sababu za udhitibiti wa mashine hizo, “I’m a father of a 12-year-old daughter and I wouldn’t want her having access to it, so we paid close attention to that.”
Source – Daily Mail

إرسال تعليق