Waendesha vyombo vya moto barabarani wamerahisishiwa njia ya
kununua na kulipia mafuta kwa njia ya M-Pesa, kufuatia ushirikiano kati
ya kampuni ya simu za mkononi Vodacom M-Pesa na kampuni ya uuzaji na
usambazaji wa mafuta ya Total Tanzania. Ushirikiano huo umeanzia kwenye
vituo vichache vya Total Tanzania na baadae kusambaa maeneo mbalimbali
nchini, lengo kuu ni kuhakikisha kila mtanzania anaemiliki chombo cha
moto anakuwa na uwezo wa kununua na kulipia mafuta kwa njia iliyo salama
na
uhakika.
uhakika.

Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim
akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya kulipia
mafuta kwa Mpesa kwenye vituo vya mafuta vya Total nchini. Kulia ni
Mkurugenzi wa Biashara wa Total Romee de Villeneuve. Uzinduzi huo
umefanyika leo jijini Dra es salaam
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom
Tanzania, Salum Mwalim, amesema siku zote kampuni yake imekuwa msitari
wa mbele katika kurahisisha maisha ya Watanzania kupitia miundombinu ya
kiteknolojia iliyo nayo.
“Tumekuwa tukibuni njia mbalimbali kila siku kwa lengo la kuwapa
urahisi wateja wetu na kuwaondolea adha ambazo wanaweza kuzipata wakiwa
wanataka kununua mafuta kutoka vituo vya Total Tanzania, sasa wateja
wetu wote kupita M-Pesa ambayo siku hizi imechukua nafasi kubwa sana
katika mfumo wa maisha ya binadamu wana uwezo wa kununua na kulipia
mafuta kutoka vituo ivyo vya mafuta,” alisema Mwalim.
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania,Salum Mwalim
akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi ya kulipia mafuta
kwa Mpesa kwenye vituo vya mafuta vya Total muda mfupi baada ya
kuzinduliwa rasmi kwa huduma hiyo kwenye kituo cha Total cha Morocco
jijini Dra es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Biashara wa Total Romee de
Villeneuve. Huduma hiyo itakuwa ikipatikana kwenye vituo vyote vya Total
hapa nchini
Aidha, Mwalim aliongeza kuwa kampuni ya Vodacom kupitia M-Pesa
wataendelea kuwaletea wateja mambo mengi ambayo hayajawahi kutokea
nchini, lengo likiwa ni kuhakikisha biashara zote nchini zimeunganishwa
na M-Pesa ili kwenda sambamba ambapo hadi sasa tayari biashara zaidi ya
320 zimeshaunganishwa na huduma hiyo.
“Tunatambua watu wengi wanahitaji la kununua mafuta kwa ajili ya
magari au piki piki zao lakini kwa bahati mbaya wanaweza kufika kwenye
kituo cha mafuta wakiwa na fedha pungufu, sasa wasiwe na wasi wasi
wowote endapo watakuwa na fedha katika akaunti zao
za M-Pesa wanaweza kutatua tatizo hilo,” alisisitiza Mwalim.
za M-Pesa wanaweza kutatua tatizo hilo,” alisisitiza Mwalim.
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim (wa pili
kushoto) akimsadia dereva Taxi Said Juma kulipia mafuta kwa njia ya
M-pesa katika kituo cha Mafuta cha Totola Morocco jijini Dar es salaam
akiwa ndie mteja wa kwanza kutumia huduma hiyo muda mfupi baada ya
kuzinduliwa kituoni hapo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara wa Total
Romee de Villeneuve na kulia ni mhudumu wa kituo hicho Malaki Peter.
Huduma hiyo itakuwa ikipatikana kwenye vituo vyote vya Total nchini
Kwa upande wake Meneja wa Maendeleo, Ubora na Mafunzo wa Kituo cha
mafuta cha Total Tanzania, Maria Lebby, Amesema kupitia njia hii wateja
wa Total watanufaika kutokana na namna kampuni hiyo ilivyo jidhatiti
katika kurahisisha njia za malipo.
“Tumekuwa tukipokea wateja mbalimbali kwa nyakati tofauti zikiwemo za
usiku ambazo ni hatarishi kwa usalama wa fedha alizobeba mteja, hivyo
basi kuanzia sasa mteja wetu anaweza kutembea bila yakubeba fedha
taslimu na badala yake kuziweka kwenye akaunti yake ya M-Pesa na
kujihakikishia anapata huduma akiwa na amani juu ya usalama wa fedha
zake.”
Mfanyakazi wa kituo cha mafuta cha Total Morocco jijini Dar es
salaam akitoa huduma ya mafuta kwa wateja. Total na Vodacom imezindua
ubia wa kibiashara unaowawezesha wateja kulipia huduma ya mafuta kwa
M-pesa kwenye vituo vyote vya Total nchi nzima. Huduma hiyo inalenga
kutoa unafuu na urahisi wa malipo kwa wateja
Aidha Meneja huyo aliendelea kubainisha manufaa watakayopata wateja
kwa kusema “huu ni wakati wakutumia teknolojia tulizonazo ili
kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa watanzania, waliowengi wanapenda
kufanya mambo yao kwa uharaka hasa wanapokuwa na majukumu mengine
yakufanya, kupitia huduma hii tatizo hilo litakuwa limetatuliwa. Natoa
wito kwa makampuni mengine kukubali kupokea mapinduzi yanayoletwa na
teknolojia ili kuweza kwenda na wakati na kurahisisha mfumo mzima wa
upatikanaji wa huduma.”
إرسال تعليق