Kanali Massawe aishukuru Vodacom kwa kuikomboa Goziba (Kagera)

 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe, amezungumzia jinsi ambavyo uboreshawaji wa huduma za mawasiliano zinavyochochea kubadili maisha ya watu kupitia kuboreka kwa shughuli za kiuchumi na kijamii huku akipongeza maamuzi ya kampuni ya Vodacom ya kupelekea mawasiliano kwenye kisiwa cha Goziba kilichopo Ziwa Victoria eneo la mkoa wa Kagera.
002 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fabian Massawe (wa tatu kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Muleba Lembris Kipuyo (wa pili kushoto) wakiwa pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom ambao baadhi yao walifundishwa na Kanali Massawe wakati alipokuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee jijini Dar es salaam.Kanali Massawe alifika Makao Makuu ya Vodacom kwa shughuli za kikazi ambapo alivuta hisia za wafanyakazi waliowahi na hata ambao hawakuwahi kupitia mikononi mwake enzi za ualimu na hivyo kuleta hali ya furaha ikitawaliwa na utani na ukumbusho wa matuko ya shule.
Kanali Masawe, ameyasema hayo wakati alipotembelea Makao Makuu ya Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom jijini Dar es salaam na kukutana na Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wake Georgia Mutagahywa ikiwa ni sehemu ya kutoa Shukurani kwa kufanikisha kuweka mnara wa simu katika kisiwa cha Goziba pamoja na kusaidia ujenzi wa kituo cha afya kisiwani humo kupitia Vodacom Foundation.
Amesema tangu Goziba ilipounganishwa kwenye mtandao wa simu za mkononi kumekuwepo na mabadiliko makubwa katika maisha ya wakazi wa kisiwa hicho huku ikisaidiwa kwa kiwango kikubwa suala la ulinzi na usalama na kuifungua Goziba. “Tunawashukuru sana Vodacom, mmekuwa wa kwanza kufikisha huduma za mawasiliano ya simu kisiwani Goziba na hivyo kuwafanya wakazi wake kuendelea kuwakumbuka kwa namna mlivyowakomboa,” alisema Massawe.
“Hali ya ulinzi na usalama kwenye kisiwa cha Goziba haikuwa nzuri hata kidogo, kisiwa kilikuwa kikibaliwa na wimbi kubwa la uvamizi wa majambazi waliokuwa wakiwavamia wavuvi na kuwapora fedha na mali zao ikiwemo nyavu na mashine za boti huku wakikosa msaaada wowote kwani kisiwa hakina kituo cha Polisi na hawkauwa na namna ya kuomba msaada kutoka Bukoba kutokana na kukosa huduma za mawasiliano.”
Pamoja na kuipongeza kampuni hiyo, Kanali Masawe amesema kuwa, huduma hizo za Mawasiliano pia zimefungua fursa za kiuchumi kwa wakazi wa kisiwa hicho ambacho sasa wanawasiliana moja kwa moja na watu walioko katika maeneo mengine ya nchi na hata nje ya Nchi hususa Nchi jirani ya Kongo ambayo wanafanya nayo biashara ya kuuza dagaa.
“Hali hii imeimarisha shughuli za uvuvi ambao ndio msingi wa maisha ya wanaGoziba kwani pia kwa sasa wanawasiliana na wachuuzi wa bara na hata nje ya nchi hususan Congo DRC ambao ni wanunuzi wakubwa wa samaki na dagaa wa kutoka Goziba na hivyo kuwa na uhakika na soko na hivyo kupunguza usmbufu na gharama za biashara, hili ni jambo litakaloendela kukumbukwa na kuheshimiwa na wana Goziba na mkoa kwa ujumla.”
Akizungumzia ujenzi wa kituo cha afya, Mkuu huyo wa Mkoa amesema kama ilivyo kwa huduma za mawasiliano, kisiwa cha Goziba hakikuwa na huduma za afya na hivyo kuwafanya wakazi wake kuishi katika mazingira magumu. Kisiwa cha Goziba kilichomo nfdanmi ya eneo la kiutawala la Wilaya ya Muleba kipo umbali wa zaidi ya Maili 20 kutoka Bukoba ikiwachukua wakazi wake safari isiyopungua
ya saa kati ya 9 hadi 10 kufika huduma za kijamii ikwemo afya.
“Tunawashukuru pia Vodacom kupitia mfuko wake wa kusaidia Jamii kwa kutusaidia kwenye ujenzi wa zahanati likiwa ni ombi la wananchi hao wakati w ahafla ya uzinduzi wa mnara. Mngeweza kusema huduma za mawasiliano zimetosha lakini mlikubali pia kusaidia ujenzi wa Zahanati ya kwanza ksiwani humo ambayo inasbiriwa kwa hamu na wananachi. Serikali ya Mkoa ina mpango wa kuipandisha hadhi Zahanati hiyo hiyo kuwa kituo cha afya pindi tu ujenzi wake utakapokamilika ili kiwe na uwezo wa kutoa huduma nyingi
na bora zaidi kwa wananchi,” aliongeza Massawe.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema kilichofanywa na Vodacom kwa watu wa Goziba cha kuwafikishia mawasiliano na huduma za afya ni jambo lililoacha alama kwa wakazi wa Goziba na Kagera kwa ujumla. Ni upendo wa hali ya juu wa kampuni kwa wananchi wanaowzunguka ni vema wengine wakaona kazi hii kubwa na nzuri ya Vodacom ili nao wajitoe kwa jamii ikiwemo za pembezoni ambazo zinakabiliwa na changamoto mbalimbali za kijamii.”
Kisiwa cha Goziba bado hakina shule na kituo cha polisi.

Post a Comment

Previous Post Next Post