Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe,
amezungumzia jinsi ambavyo uboreshawaji wa huduma za mawasiliano
zinavyochochea kubadili maisha ya watu kupitia kuboreka kwa shughuli za
kiuchumi na kijamii huku akipongeza maamuzi ya kampuni ya Vodacom ya
kupelekea mawasiliano kwenye kisiwa cha Goziba kilichopo Ziwa Victoria
eneo la mkoa wa Kagera.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fabian Massawe (wa tatu kushoto) na Mkuu
wa Wilaya ya Muleba Lembris Kipuyo (wa pili kushoto) wakiwa pamoja na
baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom ambao baadhi yao walifundishwa na
Kanali Massawe wakati alipokuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee
jijini Dar es salaam.Kanali Massawe alifika Makao Makuu ya Vodacom kwa
shughuli za kikazi ambapo alivuta hisia za wafanyakazi waliowahi na hata
ambao hawakuwahi kupitia mikononi mwake enzi za ualimu na hivyo kuleta
hali ya furaha ikitawaliwa na utani na ukumbusho wa matuko ya shule.
Kanali Masawe, ameyasema hayo wakati alipotembelea Makao Makuu ya
Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom jijini Dar es salaam na kukutana na
Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wake Georgia Mutagahywa ikiwa ni
sehemu ya kutoa Shukurani kwa kufanikisha kuweka mnara wa simu katika
kisiwa cha Goziba pamoja na kusaidia ujenzi wa kituo cha afya kisiwani
humo kupitia Vodacom Foundation.
Amesema tangu Goziba ilipounganishwa kwenye mtandao wa simu za
mkononi kumekuwepo na mabadiliko makubwa katika maisha ya wakazi wa
kisiwa hicho huku ikisaidiwa kwa kiwango kikubwa suala la ulinzi na
usalama na kuifungua Goziba. “Tunawashukuru sana Vodacom, mmekuwa wa
kwanza kufikisha huduma za mawasiliano ya simu kisiwani Goziba na hivyo
kuwafanya wakazi wake kuendelea kuwakumbuka kwa namna mlivyowakomboa,”
alisema Massawe.
“Hali ya ulinzi na usalama kwenye kisiwa cha Goziba haikuwa nzuri
hata kidogo, kisiwa kilikuwa kikibaliwa na wimbi kubwa la uvamizi wa
majambazi waliokuwa wakiwavamia wavuvi na kuwapora fedha na mali zao
ikiwemo nyavu na mashine za boti huku wakikosa msaaada wowote kwani
kisiwa hakina kituo cha Polisi na hawkauwa na namna ya kuomba msaada
kutoka Bukoba kutokana na kukosa huduma za mawasiliano.”
Pamoja na kuipongeza kampuni hiyo, Kanali Masawe amesema kuwa, huduma
hizo za Mawasiliano pia zimefungua fursa za kiuchumi kwa wakazi wa
kisiwa hicho ambacho sasa wanawasiliana moja kwa moja na watu walioko
katika maeneo mengine ya nchi na hata nje ya Nchi hususa Nchi jirani ya
Kongo ambayo wanafanya nayo biashara ya kuuza dagaa.
“Hali hii imeimarisha shughuli za uvuvi ambao ndio msingi wa maisha
ya wanaGoziba kwani pia kwa sasa wanawasiliana na wachuuzi wa bara na
hata nje ya nchi hususan Congo DRC ambao ni wanunuzi wakubwa wa samaki
na dagaa wa kutoka Goziba na hivyo kuwa na uhakika na soko na hivyo
kupunguza usmbufu na gharama za biashara, hili ni jambo litakaloendela
kukumbukwa na kuheshimiwa na wana Goziba na mkoa kwa ujumla.”
Akizungumzia ujenzi wa kituo cha afya, Mkuu huyo wa Mkoa amesema kama
ilivyo kwa huduma za mawasiliano, kisiwa cha Goziba hakikuwa na huduma
za afya na hivyo kuwafanya wakazi wake kuishi katika mazingira magumu.
Kisiwa cha Goziba kilichomo nfdanmi ya eneo la kiutawala la Wilaya ya
Muleba kipo umbali wa zaidi ya Maili 20 kutoka Bukoba ikiwachukua wakazi
wake safari isiyopungua
ya saa kati ya 9 hadi 10 kufika huduma za kijamii ikwemo afya.
ya saa kati ya 9 hadi 10 kufika huduma za kijamii ikwemo afya.
“Tunawashukuru pia Vodacom kupitia mfuko wake wa kusaidia Jamii kwa
kutusaidia kwenye ujenzi wa zahanati likiwa ni ombi la wananchi hao
wakati w ahafla ya uzinduzi wa mnara. Mngeweza kusema huduma za
mawasiliano zimetosha lakini mlikubali pia kusaidia ujenzi wa Zahanati
ya kwanza ksiwani humo ambayo inasbiriwa kwa hamu na wananachi. Serikali
ya Mkoa ina mpango wa kuipandisha hadhi Zahanati hiyo hiyo kuwa kituo
cha afya pindi tu ujenzi wake utakapokamilika ili kiwe na uwezo wa kutoa
huduma nyingi
na bora zaidi kwa wananchi,” aliongeza Massawe.
na bora zaidi kwa wananchi,” aliongeza Massawe.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema kilichofanywa na Vodacom kwa watu wa Goziba
cha kuwafikishia mawasiliano na huduma za afya ni jambo lililoacha
alama kwa wakazi wa Goziba na Kagera kwa ujumla. Ni upendo wa hali ya
juu wa kampuni kwa wananchi wanaowzunguka ni vema wengine wakaona kazi
hii kubwa na nzuri ya Vodacom ili nao wajitoe kwa jamii ikiwemo za
pembezoni ambazo zinakabiliwa na changamoto mbalimbali za kijamii.”
Kisiwa cha Goziba bado hakina shule na kituo cha polisi.
إرسال تعليق