Taifa Stars |
LICHA
ya kuambulia sare ya 1-1 ugenini na Namibia mwezi uliopita, Tanzania
imezidi kuporomoka kwenye orodha ya viwango vya soka vya FIFA baada ya
kushuka kwa nafasi tano toka nafasi yake ya awali.
Kwa mujibu wa orodha mpya ya FIFA, Tanzania sasa imeporomoka hadi nafasi ya 122 toka 117 iliyokuwa inaishikilia katika orodha ya Machi ikiwa nyuma ya Malawi iliyo katika nafasi ya 121.
Pia imeizidi kidogo tu nchi iliyo kwenye vita vya muda mrefu Afghanistan waliopo kwenye nafasi ya 123 ambayo haina mvuto mkubwa katika soka.

Nchi zilizo chini ya Tanzania ambazo
zinatokea Afrika Mashariki na Kati ni Burundi iliyo katika nafasi ya 125 baada
ya kupanda nafasi nne, wakati Rwanda iko namba 129 baada ya kukwea nafasi tano
juu.
Kenya iko katika nafasi ya 106 baada ya
kupanda nafasi tatu, Sudan nafasi ya 117, Ethiopia wanashika 101 wakati Waganda
ndiyo wanaonekana vinara katika ukanda huu kwa kuwa wako 86 huku wakiwa
wameporomoka nafasi moja tu.
Katika
orodha ya Dunia, Hispania imeendelea kuongoza ikifuatiwa na Ujerumani,
Ureno ikiwa nafasi ya tatu na kufuatiwa na Colombia, Uruguay na
Argentina wakati wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia, Brazili
wanakamata nafasi ya sita kisha Uswisi, Italia na Ugiriki imefunga dimba
la 10 Bora.
Post a Comment