Mtoto mzuri kutoka Jumba la Vipaji Tanzania (THT), Winfrida Josephat ‘Recho THT’ |
MALOVEE? Bosi
wa Top Band, Khaleed Mohamed ‘TID’ au ‘Mzee Mnyama’ na mtoto mzuri
kutoka Jumba la Vipaji Tanzania (THT), Winfrida Josephat ‘Recho THT’,
wanadaiwa kuwa na uhusiano uliotafsiriwa ni wa kimapenzi, Ijumaa
Wikienda limeinusa.
Kwa
mujibu wa chanzo makini, wawili hao wamekuwa wakionekana pamoja sehemu
mbalimbali huku wakidaiwa kupiga ‘mitungi’ kiasi cha kushindwa kuzificha
hisia zao.
Bosi wa Top Band, Khaleed Mohamed ‘TID’ au ‘Mzee Mnyama’.
“Mbona
ipo wazi, TID na Recho siku hizi hawafichi kitu, tena wanapopiga
mitungi ndiyo kabisa, mfano mzuri ni juzikati walikuwa pamoja mjini
Dodoma, waliponda raha kinomanoma,” kilitiririka chanzo hicho.
Kama
ilivyo ada, wanahabari wetu waliingia mzigoni kwa kuanzia nyumbani kwa
Recho, Kinondoni, Dar, wakamkosa lakini badala yake, walipatikana
mashosti zake wa karibu. “Recho
kwa sasa anatoka na Mnyama na hapa tunavyoongea yupo Njombe ambapo
ametimka baada ya taarifa za yeye kutoka na TID kuzagaa mtaani, halafu
pia Recho siku hizi anapombeka sana na tunahisi hata ‘mambo meupe’
anatumia,” alisema shosti huyo.Baada
ya kushibishwa data hizo, waandishi wetu walitinga ofisini kwake THT,
Kinondoni ambapo wanamuziki wenzake walisema staa huyo ana muda mrefu
hajafika kazini hapo pasipo kutoa sababu za msingi. Ijumaa Wikienda lilimpigia simu Recho, akafunguka:
“Kweli
nakunywa pombe lakini si kiivyo watu wanavyonisema. TID ni mtu wangu
kikazi wala siyo kimapenzi. Watu wamekuwa wakinishutumu kila ninapokuwa
na mwanaume wanasema ni bwana’ngu kitu ambacho si cha kweli kama
wanavyonizushia kuvuta bangi. “THT
siendi kwa sababu nimesafiri, hapa ninapoongea nipo Njombe. Nimekuja
kutulia huku kutokana na maneno kuzidi na watu kunipakazia uongo,”
alisema Recho. Kwa upande wake TID, alipopigiwa simu, alijitetea kwa kusema kuwa yupo na Recho kikazi na wala si vinginevyo. “Dah...!
Ebwana naomba uachane na hizo habari za mapenzi, mimi ni mtu mzima nina
mengi ya maendeleo ambayo natakiwa nifanye,” alisema TID.
Source: Gpl
Post a Comment