
Baadhi ya wanariadha walioshiriki katika mashindano ya Boston.
Mmarekani mweusi, Meb Keflezighi, mzaliwa wa
Eritrea ndiye mshindi wa mbio za nyika za Boston Marekani huku Rita
Jeptoo wa Kenya akishinda mbio hizo upande wa wanawake.
Mbio hizo zimefanyika mwaka mmoja baada ya ule mkasa wa shambulizi la bomu ambako watu watatu waliuawa na wengine kujeruhiwa.
Hata hivyo washiriki walionyesha ujasiri kwa
kujitokeza kwa wingi. Washindani zaidi ya elfu thelathini na sita
wameshiriki kufanikisha mbio hizo huku ulinzi ukiwa imarishwa kweli
kweli.
Ilikuwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha
miaka 30 ambapo Mmarekani ameshinda tena mbio hizo. Meb pia ni bingwa wa
zamani wa mbio za marthon ya New york na pia za olympiki.
Katika soka Manchester city sasa iko pointi sita
nyuma ya viongozi wa ligi ya Uingereza Liverpool baada ya kujipatia
ushindi wa mabao tatu kwa moja katika mechi yao dhidi ya west Brom na
kuongeza matumaini ya kujipatia kombe hilo iwapo Liverpool itateleza
katika mechi zake zijazo .
Manchester City wako katika nafasi ya tatu
wakiwa pointi moja tu nyuma ya Chelsea iliyo katika nafasi ya pili, na
pointi sita nyuma ya liverpool inayoongoza katika orodha ya ligi ya
premier.
Samuel Eto'o hatashiriki mechi muhimu ya nusu
fainali ya champions league ambapo timu ya Chelsea inatarajiwa kukutana
na Atletico Madrid kufuatia jeraha la goti.
Mechi hiyo itachezwa siku ya jumanne huko Uhispania.
Eto'o ndiye aliyefunga bao la pekee katika mechi
ya jumamosi ambapo Chelsea walilalazwa 2-1 na klabu ya Sunderland iliyo
ya mwisho kwenye orodha
إرسال تعليق