Vitendo vya mapenzi ya jinsia moja vinapingwa sana katika mataifa ya Afrika. Serikali
ya Tanzania imefutilia mbali usajili wa shirika moja lisilokuwa la
kiserikali kwa sababu ya kuhamasisha mapenzi ya jinsia moja katika
jamii. Shirika hilo kwa jina Sisi Kwa Sisi lilisajiliwa baada ya kudai kuwa malengo yake yalikuwa ni kusaidia jamii. Tanzania
imesema imechukua hatua ya kufutilia mbali usajili wa shirika hilo kwa
kukiuka sheria za nchi na kwenda kinyume na malengo ya usajili wake.
Mkurugenzi
wa usajili wa mashirika yasiyo ya Kiserikali nchini Tanzania, Maseli
Katemba, amesema kuwa shirika hilo la Sisi kwa Sisi limekiuka malengo
yake ya awali ya kuwapa elimu na misaada ya kifedha wananchi lakini
mambo yakawa tofauti. "Baada ya kufuatilia tumegundua kuwa sasa wanatilia mkazo kuwasaidia watu wa jinsia moja," alisema Bwana Katemba.Bwana
Katemba amesema kuwa Serikali itaendelea na kuyasaka makundi mengine
kama hayo ambayo yanaendesha maswala yaliyo kinyume na sheria za
Tanzania. Source: BBC |
إرسال تعليق