Licha tatizo la usambazaji wa album bongo lililowafanya wasanii
wengi kusitisha kutoa albums kwa kuhofia kupata hasara, rapper Joseph
haule aka Professor Jay ameahidi kutoa album mpya mwaka huu (2014),
ambayo itakuwa ni album yake ya tano.
Rapper huyo mkongwe ambaye hivi karibuni ametoa single mpya
iitwayo ‘Kipi sijasikia’, amesema ana mpango wa kutumia njia walizotumia
Lady Jaydee na Mrisho Mpoto katika kusambaza album zao zilizopita,
kusambaza album yake mpya itakayoitwa ‘Izack mangesho’.
“Kweli sasa hivi kwa wadosi pale kunasumbua…lakini tuna mpango wa kuongea pia na Max Malipo”, amesema Professor Jay kupitia Magic Fm. “Unajua
Max Malipo wapo karibu kila sehemu kwahiyo wanaweza kusambaza kazi
zetu. Kama Mrisho Mpoto alianza kuuza album yake kwa style hiyo..hata
dada Jaydee pia naona aliiuza mwenyewe kwa style hiyo..so na mimi
nadhani naweza kupitia njia hiyo lakini kwa kuiboresha zaidi”.
Album za Professor Jay zilizopita ni ‘Machozi Jasho na Damu- 2001’,
‘Mapinduzi Halisi -2003’, ‘J.O.S.E.P.H- 2006’, na ‘Aluta Continua
-2007’.

Post a Comment