Rais Kikwete na Rais wa Zanzibar waongoza mamia kumuombea dua Abeid Karume.


 

Rais Jakaya Kikwete na rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein  jana  wamewaongoza mamia ya wananchi katika dua maalum ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi marehemu  Abeid Amani Karume.
 
Karume aliuawa April 7 mwaka 1972 akiwa katika jengo lililokuwa Makao Makuu ya Chama cha Afro Shirazi huko Kisiwandui mjini Unguja wakati huo ambalo sasa ni Ofisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi- Zanzibar.
 
Viongozi wengine waliohudhuria dua hiyo ni pamoja na Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi na Rais Mstaafu wa Zanzibar Awamu ya Sita Dk. Amani Abeid Amani Karume.

 
Katika kiwanja cha Ofisi Kuu ya CCM dua zilisomwa na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini na baadae viongozi pamoja na watu wengine walioteuliwa walikwenda kwenye kaburi la marehemu ambako waliweka mashada ya maua

Post a Comment

Previous Post Next Post