![DSC00207](http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2014/04/DSC002073.jpg)
AJALI
HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 27.04.2014 MAJIRA YA SAA 22:45 USIKU HUKO
KATIKA KIJIJI CHA MAKONGOLOSI, KATA YA MAKONGOLOSI, TARAFA YA KIWANJA,
BARABARA YA MAKONGOLOSI/MKWAJUNI, WILAYA YA CHUNYA. AIDHA KATIKA AJALI
HIYO WATU WAWILI WALIJERUHIWA 1. FARAHAD ABDUL (26) DEREVA WA GARI HILO
AMBAYE AMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA NA RAYMOND SIKAONA (29)
MFANYAKAZI KATIKA HALMASHAURI YA MJI MDOGO WA MAKONGOLOSI AMBAYE ALIKUWA
ABIRIA NA AMELAZWA HOSPITALI YA MWAMBANI. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO
KASI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA JAPO KUWA AMELAZWA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA
MOTO KWA KUZINGATIA NA KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI
KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA.
KATIKA MISAKO:
KATIKA
MSAKO WA KWANZA ULIOFANYIKA HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA SANGAMBI,
TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA MTU MMOJA AITWAE
JAPHET NZOWA (39) MFANYABIASHARA, MKAZI WA SANGAMBI AKIWA NA POMBE
KALI[VIROBA] ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI AINA YA BOSS PAKETI 173
NA RIDDER PAKETI 60.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 28.04.2014 MAJIRA YA SAA 12:30 MCHANA.
MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIZO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI
ZINAENDELEA.
KATIKA
MSAKO WA PILI ULIOFANYIKA HUKO KATIKA KIJIJI CHA SHOGA, KATA YA
SANGAMBI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MFANYABIASHARA MMOJA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JOHN DAWILO (29) MKAZI WA SHOGA AKIWA NA POMBE
KALI[VIROBA] ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI AINA YA BOSS PAKETI 61
NA RIDDER PAKETI 15.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 28.04.2014 MAJIRA YA SAA 10:00 ASUBUHI.
MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIZO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI
ZINAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA KUACHA KUUZA BIDHAA
ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa na:-
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
إرسال تعليق