Umeboreka na kazi? Fahamu namna ya kujiwekea changamoto kazini.

woman-on-cellphone
0

Kama unafikiri kama mimi kwamba kukaa na kuangalia mambo yanavyokwenda, hicho kitu mimi binafsi sikipendi. Ninapenda kuona kuna changamoto na ninafanya kazi kwa ufanisi kila siku. Ila kama umefikia eneo ambalo mambo hayaendi , mambo yanakuboa unatakiwa usiboreke. Amsha nguvu zako kwa upya tena, kwani shauku yako ya kazi itafanya hali yako ya kazi iwe bora zaidi. Unapohusisha hisia zako na kazi yako, utajikuta ukipenda kazi na kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ya ziada huku ukiwa na furaha na hicho kitu kukufanya uwe na mafanikio bora. Unaweza kujua ninaelekea  wapi? Wewe mwenyewe ndio chanzo cha furaha kazini, kama uliweza kusoma makala yangu hapo nyuma je ungependa kufurahia kazi yako tena?
Acha kuota ndoto za mchana, simama na uchukue majukumu na uyakabili ipasavyo;

1. Badilisha mtazamo wako: Fanya kana kwamba unamiliki hiyo kampuni

Weka changamoto ya kufanya kazi kama kampuni ni ya kwako” utajiona ukifanya kazi bila kuchoka au kukata tamaa, hivyo kukufanya hata utakapo miliki kampuni yako utafanya vizu vizuri zaidi. Kama unafanya kazi zako mwenyewe utakuwa na hali ya kufanya kazi kwa juhudi bila kuboreka, kwani unataka kuona kampuni inafika mahali fulani.

2. Kazi zinazoboa zitengenezee program ambazo zitasaidia zijiendeshe zenyewe

Kama unafanya kazi ya kujirudia kila siku, tafuta mfumo wa komputa ambao utarahishisha utendaji wa kazi hiyo. Kama unafanya kila siku kitu hicho hicho inamaanisha kuna namna ambayo unaweza kukifanya kitu hicha na kikaweza kufanyika bila ya  wewe kuboreka. Inamaanisha tumia akili nyingi kuliko nguvu, fuatilia kwenye teknolojia kazi hiyo inaweza kufanyika vipi?
3. Jiunge na timu nyingine
Jaribu kuongea na wafanyakazi wenzako wenye ujuzi tofauti na wa kwako, wanaweza kukusaidia na kuongeza ujuzi wa namna ya kufanya kazi hiyo kwa ubora na urahisi zaidi. . Hata kama wazo limetoka kitengo tofauti na cha kwako na wakakataa kwa sababu ya bajeti, ila mtu mwenyewe ukiweza kuhakikisha jambo hilo linatokea linakuwekea changamoto furaha ya kuona likitokea.

4. Badilisha kazi yako kuwa kama ni mchezo.

Kama ukicheza mchezo wa komputa unatamani kufikia kiwango fulani cha pointi, vivyo hivyo katika kazi hakikisha unafikia viwango fulani kila siku

5. Jifunze ujuzi mpya

Hakikisha unachokifanya ujue kuna ujuzi gani mpya umeingia kuhusiana na kile unachokifanya,jifunze na ufanyie kazi.

6. Tengeneza malengo ya kazi yako kila siku na uyafikie.

Inawezekana unaboreka kwa sababu huna malengo ya kazi kila siku. Upo opo tu, unaingia na kutoka ofisini bila kujua leo umefanya nini na ulitakiwa kufanya nini? Hujui unaweza kufanya kitu gani? Jiwekee changamoto malengo katika kazi kila siku, utaona mambo yakianza kwenda tofauti.

7. Kumbuka:  Jambo kufanyika ni vizuri zaidi kuliko kusema mambo yamekwenda vizuri

Inawezekana unaboreka kwa sababu unaogopa kushindwa, unasubiri wakati muafaka na wazo zuri hivyo unashindwa kuanza jambo kwa sababu unaona bado. Ukiondoa woga, hofu ,mashaka na wasiwasi ukaamua kufanya, jambo litafanyika. Naamini umepata changamoto za kukusaidia kwa kiasi fulani, kama una maoni au ushauri usisite kutuandikia

Post a Comment

Previous Post Next Post