Kama unafikiri kama mimi kwamba kukaa na kuangalia mambo
yanavyokwenda, hicho kitu mimi binafsi sikipendi. Ninapenda kuona kuna
changamoto na ninafanya kazi kwa ufanisi kila siku. Ila kama umefikia
eneo ambalo mambo hayaendi , mambo yanakuboa unatakiwa usiboreke. Amsha
nguvu zako kwa upya tena, kwani shauku yako ya kazi itafanya hali yako
ya kazi iwe bora zaidi. Unapohusisha hisia zako na kazi yako, utajikuta
ukipenda kazi na kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ya ziada huku ukiwa
na furaha na hicho kitu kukufanya uwe na mafanikio bora. Unaweza kujua
ninaelekea wapi? Wewe mwenyewe ndio chanzo cha furaha kazini, kama
uliweza kusoma makala yangu hapo nyuma je ungependa kufurahia kazi yako
tena?
Acha kuota ndoto za mchana, simama na uchukue majukumu na uyakabili ipasavyo;
1. Badilisha mtazamo wako: Fanya kana kwamba unamiliki hiyo kampuni
Weka changamoto ya kufanya kazi kama kampuni ni ya kwako” utajiona
ukifanya kazi bila kuchoka au kukata tamaa, hivyo kukufanya hata utakapo
miliki kampuni yako utafanya vizu vizuri zaidi. Kama unafanya kazi zako
mwenyewe utakuwa na hali ya kufanya kazi kwa juhudi bila kuboreka,
kwani unataka kuona kampuni inafika mahali fulani.
2. Kazi zinazoboa zitengenezee program ambazo zitasaidia zijiendeshe zenyewe
Kama unafanya kazi ya kujirudia kila siku, tafuta mfumo wa komputa
ambao utarahishisha utendaji wa kazi hiyo. Kama unafanya kila siku kitu
hicho hicho inamaanisha kuna namna ambayo unaweza kukifanya kitu hicha
na kikaweza kufanyika bila ya wewe kuboreka. Inamaanisha tumia akili nyingi kuliko nguvu, fuatilia kwenye teknolojia kazi hiyo inaweza kufanyika vipi?
3. Jiunge na timu nyingine
Jaribu kuongea na wafanyakazi wenzako wenye ujuzi tofauti na wa
kwako, wanaweza kukusaidia na kuongeza ujuzi wa namna ya kufanya kazi
hiyo kwa ubora na urahisi zaidi. . Hata kama wazo limetoka kitengo
tofauti na cha kwako na wakakataa kwa sababu ya bajeti, ila mtu mwenyewe
ukiweza kuhakikisha jambo hilo linatokea linakuwekea changamoto furaha
ya kuona likitokea.
4. Badilisha kazi yako kuwa kama ni mchezo.
Kama ukicheza mchezo wa komputa unatamani kufikia kiwango fulani cha
pointi, vivyo hivyo katika kazi hakikisha unafikia viwango fulani kila
siku
5. Jifunze ujuzi mpya
Hakikisha unachokifanya ujue kuna ujuzi gani mpya umeingia kuhusiana na kile unachokifanya,jifunze na ufanyie kazi.
6. Tengeneza malengo ya kazi yako kila siku na uyafikie.
Inawezekana unaboreka kwa sababu huna malengo ya kazi kila siku. Upo
opo tu, unaingia na kutoka ofisini bila kujua leo umefanya nini na
ulitakiwa kufanya nini? Hujui unaweza kufanya kitu gani? Jiwekee
changamoto malengo katika kazi kila siku, utaona mambo yakianza kwenda
tofauti.
7. Kumbuka: Jambo kufanyika ni vizuri zaidi kuliko kusema mambo yamekwenda vizuri
Inawezekana unaboreka kwa sababu unaogopa kushindwa, unasubiri wakati
muafaka na wazo zuri hivyo unashindwa kuanza jambo kwa sababu unaona
bado. Ukiondoa woga, hofu ,mashaka na wasiwasi ukaamua kufanya, jambo
litafanyika. Naamini umepata changamoto za kukusaidia kwa kiasi fulani,
kama una maoni au ushauri usisite kutuandikia
إرسال تعليق