Mwanamitindo na mtangazaji wa TV nchini, Jokate Mwegelo
amefunguka kwa kusema kuwa ameamua kufungua biashara ya ndala za brand
yake ya ‘Kidoti’ kutokana na mapenzi yake ya uvaaji wa ndala kataki
maisha yake ya kawaida .
“Mimi napenda kuvaa ndala, napenda kuvaa wakati nakwenda
kushoot,siwezi kuvaa high hills wakati nashoot, wakati unapakwa make up
unaonaee, unatengenezwa nywele, you cannot wear hills lazima uwe umevaa
kitu comfortable,” Jokate ameiambia Bongo5.
“Kwahiyo nikaona kwamba ndala ni kitu kizuri,napenda kuvaa ndala,ni
kitu easy,kuvaa rahisi halafu ni kitu ambacho watu wanakihitaji why not
have ndala ambazo zina mvuto wa kipekee? Kama nilivyohaidi watu kwamba
Jokate kupitia brand ya Kidoti itaanzisha bidhaa mbalimbali kukidhi
mahitaji ya watu na jamii mzima. Nashukuru kuna support kwa Kidoti
yenyewe kama brand. Kwahiyo tutaendelea kutoa vitu mbalimbali vya
kufurahisha. Unajua kutoa surprise ni njia moja wapo ya kufurahisha,
hawakutegemea kupata kitu kuzuri lakini wamekipata. Kwahiyo ni mambo ya
Kidoti hayo ni bidhaa nzuri waipokee na tutaendelea kutoa bidhaa
mbalimbali.” aliongeza.
Pia Kidoti amesema kuwa bidhaa ya ndala ya Kidoti itapatikana Tanzania nzima.
“Tutasambaza Dar es salaam nzima na mikoani,kwahiyo ni kitu ambacho
kipo katika mipangilio ya kusambambaza sehemu mbalimbali ili upatikanaji
uwe rahisi na tunafanya jitihada za kutangaza sehemu ambazo zitakuwa
zinapatikana.”
إرسال تعليق