Waziri
wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe akizungumza
na wanamichezo wanaoenda kuweka kambi katika nchi za New Zealand,
Ethiopia, China na Uturuki ikiwa ni maandalizi ya mashindano ya Jumuiya
ya Madola mapema mwezi julai. Kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya
Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leornard
Thadeo.
Kushoto
ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Leornard Thadeo akifafanua jambo wakati wa hafla ya
kuwakabidhi bendera wanamichezo wanaokwenda nje ya nchi kwa ajili ya
maandalizi ya mashindano ya Jumuiya ya Madola leo jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Mambo ya njeya nchi na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe (wa
tatu kutoka kushoto) akifurahia mara baada ya kuwa kabidhi Bendera ya
Taifa wawakilishi wa wanamichezo wanaokwenda nchini New Zealand,
Ethiopia,China na Uturuki kwa ajili ya kujiandaa na msahindano ya
Jumuiya ya Madola. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Masuala ya Asia,
Balozi Mbelwa Kairuki, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Leornard
Thadeo, Katibu wa Kamati ya Olympic Tanzania Filbert Bayi na mwakilishi
wa wana michezo Neema Mwaisyula.
Rais
wa Shirikisho la Riadha Tanzania Anthony Mtaka akitoa neon la shukrani
kwa niaba ya wanamichezo wote wanaoshiriki maandalizi hayo.
Baadhi
ya wanamichezo na viongozi wao wakifuatilia kwa karibu hotuba ya Waziri
wa mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe (hayupo
pichani) wakati wa hafla ya kuwakabidhi Bendera ya Taifa leo jijini Dar
es Salaam.
Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Michezo Tanzania Leornard Thadeo akipeana mkono na
mwakilishi wa wana michezo wanaoenda nje ya nchi kwa ajili ya maandalizi
ya mashindano ya Jumuiya ya Madola mara baada ya kukabidhiwa Bendera ya
Taifa na Waziri wa wa Mambo ya nje ya nchi na Ushirikiano wa Kimataifa
Bernard Membe (mwenye shati la njano)
Waziri
wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe akiwa na
mchezaji wa timu ya Taifa ya kuogelea Hilal Hemed Hilal.
PICHA ZOTE NA FRANK SHIJA
إرسال تعليق