
Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva, akiruka kukwepa kwanja la beki wa
JKT Ruvu, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliomalizika
hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo
huo Yanga imeibuka na ushindi mnono wa mabao 5-1. Mabao matatu
yalifungwa na Mrisho Ngassa, katika dakika ya 7, Dakika ya 15 na Dakika
ya 48.
Mabao mengine yalifungwa na Didier Kavumbagu katika dakika ya 39 na bao
la tano likafungwa na Hussein Javu katika dakika ya 51. Kwa ushindi huo
sasa Yanga imefikisha jumla ya Pointi 49 wakiwa nyumba ya Azam Fc wenye
jumla ya Pointi 53 kwa tofauti ya 4. Bao la kufutia machozi la JKT Ruvu
lilifungwa na Nashon Naftari, katika dakika ya 83.


Sehemu ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia mchezo huo.

Didier Kavumbagu (kulia) akichanja mbuga kumtoka mchezaji wa JKT Ruvu.


Kipa wa JKT Ruvu, akijaribu kuokoa moja kati ya hatari zilizoelekezwa langoni kwake.
إرسال تعليق