Na Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu 34 wakazi wa Mji mdogo wa
Kibaigwa Kata ya Kibaigwa Wilaya ya Kongwa Mkoa wa Dodoma kwa makosa ya
kufanya fujo na kuharibu mali tukio lililotokea tarehe 05/05/2014 majira
ya saa 13:30Hrs.
Kamanada
wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID
MISIME – SACP amesema Vijana wanaokadiriwa kuwa zaidi ya miatatu
wakishirikiana na Wabeba mizigo wa Soko Kuu la Mazao la Kibaigwa,
walifanya maandamano bila kibali na kung’oa bango la Halmashauri ya
Wilaya ya Kongwa lenya tangazo la kutoruhusu wafanyabiashara kuingiza
mazao sokoni bila kulipa ushuru uliowekwa kwa mujibu wa sheria.
Viwango
vya ushuru vinavyotozwa vilipanda tangu tarehe 01.07.2013 ambapo gunia
la Kg. 100 za karanga zilipanda kutoka Tshs. 1000/= hadi Tshs 3000/=,
guina la mahindi lilipanda kutoka Tshs. 500/= hadi Tshs. 1000/=, dumu la
mafuta ya alizeti lilianza kutozwa Tshs. 500/=, gunia la mashudu
lilianza kutozwa Tshs. 1000/=, gunia la alizeti lilianza kutozwa Tshs.
1000/= ushuru ambao unapingwa na wabeba mizigo.
Vijana
hao wabeba mizigo walifanya fujo kwa kufunga barabara kuu ya Dodoma –
Morogoro kwa mawe na kuchoma mataili, pia walivamia maduka na bar za
jirani na kupora vinywaji na kuvunja majokofu.
Kamanda
MISIME amesema katika vurugu hizo walisababisha uhalibifu wa mali kwa
kushambulia magari kwa mawe likiwemo gari la Mbunge wa Tanga Mh. OMARI
NUNDU lenye namba za usajili T.419 CWC Land Cruiser Prado ambaye
aliyekuwa akienda Bungeni Dodoma, pia gari la Polisi namba PT. 0960 Land
Rover lilivunjwa kioo cha mlango wa mbele kulia na basi la Kampuni ya
Shabaha lililokuwa likitokea Mwanza kwenda Dar es Salaam lilivunjwa kioo
cha mbele.
Kamanda
MISIME amesema chanzo cha vurugu hizo ni wabeba mizigo wa soko la mazao
kibaigwa kupinga kitendo cha Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kuweka
tangazo la kutoza ushuru wa mazao sokoni hapo wakidai kwamba
linawakosesha kufanya kazi zao kwani wateja wanashindwa kuingiza mazao
sokoni na wao kukosa kazi.
Katika
hatua nyingine Jeshi la Polisi linawashikilia watu watatu kwa makosa ya
kupatikana na Mashamba ya Bangi. LEONARD S/O RAMADHANI MTWANGU, miaka
53, kabila Mgogo, Mkulima na Mkazi wa Kijiji cha Ilolo Wilaya ya
Mpawapwa alikamatwa akimiliki ekari tatu (3) za shamba la bangi kinyume
cha sheria.
Mtu wa
pili ni MATONYA S/O MPARE mwenye miaka 24, kabila Mgogo mkazi wa Kijiji
cha Matumbulu Manispaa ya Dodoma alikamatwa akimiliki nusu ekari ya
shamba la bangi kinyume cha sheria na mtu mwingine ni EMMANUEL S/O
LUHANGA mwenye miaka 45, kabila Mkaguru, Mkulima na Mkazi wa Kijiji cha
Nguji Wilaya ya Kongwa ambaye alikamatwa akimiliki ekari tatu (3) za
shamba la bangi kinyume cha sheria. Watuhumiwa wote watafikishwa
mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika na msako unaendelea.
Kamanda
MISIEME ametoa wito kwa wananchi wakazi wa Kibaigwa waache kujichukulia
sheria mkononi, wafuate taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria.
Kutokana na ushahidi uliopo wote waliohusika watakamatwa popote walipo
na watafikishwa Mahakamani kwa makosa ya Kufanya mkusanyiko bila halali,
Kuandamana bila kibali, kufunga barabara na kuharibu mali ambayo ni
makosa kisheria.
إرسال تعليق