Mmoja
wa majeruhi wa kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu la kutengenezwa
‘kienyeji’ ambao ulilipuka katika vyumba vya Hosteli za Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T), mtaa wa Gana jana usiku.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola, amesema mlipuko unaodaiwa
kutokea jana, ulitokana na kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu la
kutengenezwa ‘kienyeji’ ambao ulilipuka katika vyumba vya Hosteli za
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T), mtaa wa Gana
.
Amesema
tukio hilo limetokea jana Jumatatu Mei 5, 2014 saa mbili usiku, na
kujeruhi mtu mmoja ambaye hadi sasa anapatiwa matibabu katika Hospitali
ya Rufaa Bugando iliyopo jijini humo.
Taarifa
za awali kuhusu tukio hilo, zinaonyesha kuna watu/mtu ambao waliweka
bomu hilo katika hosteli hizo na kupelekea tukio hilo, ambapo hadi sasa
Jeshi hilo linaendelea na upelelezi na hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa
kuhusiana na tukio hilo.
إرسال تعليق