STAA wa filamu za Kibongo, Aisha Bui amepata mtoto wa kike
aliyejifungua kwa njia ya upasuaji lakini kumekuwa na usiri mkubwa
katika jambo hilo.
Staa wa filamu za Kibongo, Aisha Bui.
Akizungumza hivi karibuni, Aisha alisema anamshukuru Mungu kwa kumjaalia mtoto wa kike aliyempa jina la Saloma.
“Nimefurahi sana, kumpata mtoto ni jambo la kumshukuru Mungu na sasa
najisikia raha sana kuitwa mama,” alisema Aisha na kuongeza kuwa,
mwanaume aliyezaa naye ni mchumba wake wa siku nyingi ambaye anaishi nje
ya nchi na wanatarajia kufunga ndoa siku si nyingi.
إرسال تعليق