Baada ya kuzikonga nyoyo za mashabiki wa Dar es salaam usiku wa
kuamkia leo pale Club Billicanaz, Diamond Platnumz ameondoka nchini
alfajiri ya leo kurejea tena London, Uingereza anakotarajiwa kufanya
show nyingine usiku wa leo (May 17) akiwa na Ommy Dimpoz aliyemuacha
huko.

Platnumz aliingia nchini jana Ijumaa (May 16) akitokea Uingereza kama
alivyoahidi na kuhudhuria show ya MTV Africa Road to MAMA iliyofanyika
Club Billicanas usiku wa kuamkia leo. Akiwa London Platnumz aliahidi
kurejea nchini kwaajili ya tukio hilo muhimu, akiwa kama nominee wa tuzo
za MTV Africa (MAMA).
Platnumz ameshare picha akiwa uwanja wa ndege alipokuwa akijiandaa kucheck in mida ya saa 9 alfajiri.

إرسال تعليق