
Donald Sterling ambaye ni mmiliki wa timu ya mpira wa kikapu ya
Clippers amekataa kulipa fidia iliyoamriwa na NBA kwa kosa la kufanya
ubaguzi wa rangi wakati akiongea na mpenzi wake.
USA Today imeripoti kuwa mwanasheria wa mzee huyo tajiri, Maxwell
Blecher alimtumia barua makamu wa raisi wa NBA Rick Buchanan akieleza
kuwa bwana Donald Sterling hajafanya kosa lolote na kwamba hasitahili
adhabu yoyote.
Donald Sterling mwenye umri wa miaka 80 alikubwa na kashfa nzito
baada ya maongezi yake na mpenzi wake yaliyojaa ubaguzi wa rangi kuwekwa
kwenye mtandao maarufu wa udaku ‘TMZ’.
Bwana Donald alipofanya mahojiano na CNN alieleza kuwa anaamini
kabisa kuwa mpenzi wake alimtengenezea mtego ili afanye kosa hilo kubwa
kwa kuwa hata yeye wakati anasikiliza tena maongezi hayo hakuelewa ni
kwa nini alizungumza yote yale.
Kitendo chake kililaaniwa na watu mbalimbali huku baadhi yao wakitangaza nia ya kuinunua Clippers
إرسال تعليق