Kemikali zinazopatikana katika
baadhi ya bidhaa ambazo hutumiwa kila siku kama vile dawa ya kusugua
meno, sabuni na mafuta ya kujikinga kutokana na miale hatari ya jua
zinaweza kuharibu mbegu za uzazi za wanaume.
Kwa mara ya kwanza watafiti wanaonya kuwa bidhaa
hizo zina uwezo wa kuanthiri uwezo wa mbegu za uzazi za wanaume
kuzalisha mwanamke.
Wanasayansi hao wanasema kwamba
bidhaa hizo zina kemikali ambazo zinachangia matatizo ya uzazi kwa
wanaume katika nchi za magharibi.
Kemikali zinazopatikana katika dawa za kusugua meno zinasemekana kuharibu nguvu za mbegu za kiume kuweza kuzalisha.
Takriban mwanamume mmoja kati ya sita aliyeoa
nchini Uingereza anakumbwa na tatizo la kuzalisha na tatizo la utasa
ndio kiini kikubwa cha hali hiyo.
Uchunguzi huu ulifanywa na watafiti kutoka
Uingereza na Uholanzi na walifanyia uchunguzi kemikali 100 kila siku
huku wakigundua kuwa thuluthi moja ya kemikali hizo ziliathiri uwezo wa
Manii kufikia katika mayai ya mwanamke.
Utafiti huu uliandikwa katika jarida la afya la
EMBO na watafiti wanasema nyingi ya kemikali hizo hatari zinapatikana
katika mafuta yanayotumiwa kujizuia na miale hatari ya jua.
Kemikali nyingine inajulikana kama Triclosan, ambayo inapatikana katika sabuni na dawa ya kusugua meno.
Uchunguzi wa maabara ulionyesha kuwa kemikali hizo zinaathiri uwezo wa Manii ikitafuta mayai ya mwanamke kuweza kuizalisha.
Kadhalika kemikali hizo pia zinaharibu kabisa manii kiasi cha kukosa hisia kwa homoni za mwanamke.
Mabadiliko haya yanapotokea kwa mbegu za kiume, huifanya kuwa vigumu kuweza kuzalisha.
Watafiti hao wanasema kuwa mchanganyiko wa kemikali hizo ni hatari zaidi kwa mbegu hizo.
Kemikali hizi hujulikana kama kemikali
zinazoathiri jinsia kwa sababu ni sehemu ya kemikali zinzzoathiri homoni
za mwili wa mwanamume.
Mwaka jana shirika la afya duniani lilihusisha kemikali hizo na saratani ya matiti na pumu
إرسال تعليق